Baadhi ya Wafanya biashara wa katika soko kuu Manispaa ya iringa wamelalamikia
tabia inayofanywa na baadhi ya viongozi wa mamlaka ya vipimo kuwazuia kutumia
kipimo cha ndoo katika biashara zao.
Wakizungumza na nuru fm wafanya biashara hao wamedai kuwa wamekuwa
wakizuiwa kutumia ndoo ndogo katika kupima vitunguu kama kipimo cha mzani
wakati kuna wanyabiashara wengine nje ya soko hilo wanatumia njia hiyo.
Aidha wafanya biashara hao wamesema kuwa tangu kuanza kwa biashara hiyo
hawajawai pokea taarifa kutoka kwenye uongozi wowote kuwa kuna mabadiliko
katika upimaji wa bidhaa zao.

No comments:
Post a Comment