Latest News

Showing posts with label MAHUSIANO. Show all posts
Showing posts with label MAHUSIANO. Show all posts

Friday, July 7, 2017

Hizi ni NGUVU Kuu 7 Alizonazo Mwanamke!



1. Uwezo wa kuona na kugundua ya mbeleni (anawezakuona kisichosemwa au kitakachokuja).               Anatumia mlango wa sita wa fahamu unaoitwa EPS
2. Ananguvu ktk kinywa chake kuliko nguvu za mwili kwa mwanaume. Athari za kutotumia kinywa       chake vema ni kubwa zaidi.
3. Nguvu na uwezo wa kuendeleza uumbaji
4. Nguvu ya ushawishi
5. Nguvu na uwezo wa kustahimili. Kuvumilia. Kubeba mazito.
6. Nguvu na uwezo wa kujadili bei (bargaining power)
7. Uwezo wa kuwaathiri watoto (positively or negatively)

ILI NGUVU HII ITENDE KAZI
1. Tumia vema kinywa chako
2. Tumia vema ushawishi wako

Kutofanya Tendo la Ndoa Muda Mrefu Kuna Madhara, Soma Hapa!



Habari zenu, nimeona niwaletee hili nina imani mtajifunza hasa kwa wale wasiofahamu,Ukikaa Muda Mrefu bila Kufanya tendo la Ndoa madhara yake ni kama haya:

Hasira za mara kwa mara katika mambo madogo,kupendelea sana kuangalia picha za uchi,Kusahausahau,Kupendelea story za mapenzi,Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi (Mke),Kupenda kurukiarukia mambo ya watu wengine (tabia ya kufuatilia mambo yasiyokuhusu),Kuumwa na kichwa,Kukakamaa mgongo (wanaume),Kuingiliwa kirahisi na jini mahaba,Kupoteza umakini ktk kazi (efficiency),Siku ukikutana kimwili na mwenye virusi bila kinga utaambukizwa kirahisi mno,Waweza ku-develop tabia mpya ambayo hukuwahi kuwa nayo ili iwe mbadala

Ukiwa na Tabia hizi 7, Lazima Mwanaume Akukimbie



1. CHOKOCHOKO
Wanaume wengi huwa hawapendi chokochoko. Hawapendi mwanamke ambaye yeye kila wakati ni kuanzisha chokochoko ambazo zinazalisha ugomvi. Wanaume wengi hawapendi mabishano. Hawapendi ugomvi hivyo mwanamke anapokuwa hodari wa kuleta chokochoko, huepukwa.

Ni vyema basi mwanamke akachunga kauli. Akawa si mtu wa kuchimbachimba vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Asiwe na kisirani. Kinywa chake kitawaliwe na maneno matamu, yatakayomtia moyo mpenzi wake, yatakayomfariji na yatakayomfanya apende kuzungumza naye.

Mara nyingi mwanaume akiona mke au mpenziwe ni mtu wa kupenda chokochoko, mara nyingi humuepuka. Anajitahidi kadiri ya uwezo wake kukaa naye mbali. Ataona ni bora achelewe kurudi nyumbani akakutane na marafiki baa, wapige stori ili muda uende na akirudi nyumbani asiwe na muda wa kuzungumza na mwenzi wake, yeye ni kula na kulala.

2. KUTORIDHIKA
Wanaume wengi wanachukia kuwa na wanawake wasioridhika. Baadhi ya wanawake hata uwape nini huwa hawaridhiki. Wanawasumbua wapenzi wao kwamba hawawatimizii mahitaji. Mwanaume anajitoa kumpa zawadi mpenzi wake, haridhiki tu.

Anaanza kuikosoa. Anasema haifanani na yeye, eti si ya hadhi yake. Akipewa fedha anasema hazitoshi. Kila siku ni malalamiko. Hampi nafasi mpenzi wake ya kufurahia uhusiano wao.  Anamfanya kila anapokutana naye awaze atapigwa mzinga.

Bahati mbaya sasa kila atakachopewa haridhiki. Anatamani kikubwa zaidi. Wanaume wengi siku hizi wanaichukia tabia hiyo. Hawapendi kuwa na mwanamke ambaye haridhiki na kile kidogo walichojaliwa. Wanaume wengi wakiona hivyo huwa wanaanza kumuepuka mwanamke wa ‘sampuli’ hiyo.

Kwake kunakuwa hakuna jema. Badala ya kumshauri mpenzi wake mbinu za kujikwamua kiuchumi yeye ni lawama tu. Kila siku analalamika kwamba wanaume wengine wanawapa wapenzi wao mahitaji muhimu lakini wa kwake hamtimizii.

Mwanaume akiona kila analofanya kwa mpenzi au mkewe haridhiki, hatoi shukurani ni rahisi kupunguza mapenzi kwa mtu wake. Taratibu anaanza kujitoa na hata kuhamishia mapenzi kwa mtu mwingine ambaye atakuwa anaridhika kwa kidogo anachopewa. Ni muhimu kuridhika.

3. KULINGANISHA
Hii nayo ni tabia isiyopendwa na wanaume wengi. Wanaume wanapenda kuishi maisha yao. Wanapenda kuheshimiwa na wapenzi wao. Wanapenda kumsikia mwanamke akisema; ‘hakuna mwanaume mwingine wa kufanana na wewe.’

Mwanaume anapenda kuhakikishiwa kwamba hakuna mwanaume mwingine kama yeye. Yeye ndiye mzuri au bora kuliko wanaume wengine hivyo mwanamke anapoanza kuonesha tabia za kumlimnganisha na mwanaume mwingine linakuwa tatizo kubwa.

Mwanaume anakasirika. Anaona ni rahisi mwanamke wake kumtamani mtu mwingine baki kuliko yeye. Sifa anazozitoa kwa mwanaume mwingine ni nzuri hivyo zinamvutia. Kama zinamvutia siku yoyote anaweza kushawishika kumfuata yule anayemvutia.

Wanawake wanapaswa kuwa makini katika eneo hilo. Hata kama umeona kuna kitu kizuri kimekuvutia kutoka kwa mwanaume mwingine, kamwe usije kumwambia mwenzi wako. Baki nalo moyoni. Jipe moyo kwamba mwanaume uliyenaye ndiye bora kuliko wanaume wote duniani.

4. KUWA TEGEMEZI
Wakati mwingine hata kama huna kitu lakini mwanamke unashauriwa kutojionesha huna kitu. Jioneshe kwamba una kitu hata kama huna. Wanaume wa sasa hawapendi kuwa na mwanamke ambaye kila kitu anategemea kutoka kwa mwanaume.

Hata kama huna kazi lakini ni vyema basi mwanamke akajaribu kufanya biashara ndogondogo ambazo zitampunguzia mwanaume wake makali ya kuombwa fedha kila wakati. Wanaume wanapenda kuwapa wapenzi wao fedha lakini inapozidi kipimo inageuka kuwa kero.

Yani kuanzia mahitaji ya kila siku, saluni, mavazi, ada ya watoto na mengine mengi mwanamke anamtegemea mwanaume. Yeye hataki kujishughulisha hata kidogo. Anataka aletewe, kazi yake kubwa ni kulea familia nyumbani.

Mwanaume akigundua mwanamke ni tegemezi mkiwa katika hatua za mwanzoni, ni rahisi kumkimbia mwanamke na kwenda kwa mwanamke ambaye angalau atakuwa hamtegemei kwa kila kitu. Mwanamke anayejiongeza hata kwa kutoa wazo la kuanzishiwa biashara ambayo itamfanya asiwe tegemezi.

5. KUTOKUA MUELEWA
Mwanaume anapenda mwanamke muelewa. Hapendi mwanamke mbishi. Anatamani kuwa na mwanamke ambaye akimueleza kitu, anajiongeza na kufanya zaidi ya pale mwanaume alipofikiria. Mwanaume anapenda mwanamke atakayeanzisha wazo la kimaendeleo na kumshirikisha mpenzi wake ili walifanye.

Wanaume wanapenda wanawake wanaowaelewa. Kama mwanamke anakuwa si wa kumuelewa mpenzi wake, kumsaidia basi mara nyingi mwanaume humkimbia.

6. KUJITAPA KWA KUWA NACHO
Hakuna mwanaume anayependa kutawaliwa. Wanawake wenye fedha mara nyingi wanakuwa na tabia ya kutaka kuwatawala wanaume. Anataka mwanaume afanye kile ambacho yeye anataka. Fedha zinamvimbisha kichwa na kuona kwamba anaweza kuwa na mamlaka ya kumuamrisha mumewe.

Anatumia fedha zake kama fimbo ya kumchapia mpenzi wake. Ni vigumu sana wanaume kumvumilia mwanamke wa aina hiyo, mara nyingi wanajiepusha naye. Kwa kutumia fedha zake anaweza kupata mwanaume mwingine lakini pia watashindwana katika suala la kumtawala.

7. KUWA BIZE SANA
Wanaume wengi hawapendi mwanamke tegemezi lakini pia wanaume haohao wanachukia mwanamke akiwa bize sana na kazi zake. Mwanaume hapendi kuona mwenzi wake anakuwa bize na kazi au biashara zake kiasi ambacho kitamfanya hata akose muda na mwenzi wake.

Unachotakiwa kufanya hapo mwanamke ni kujigawa. Hakikisha unakuwa bize na kazi lakini si ya kupitiliza maana itamfanya mwanaume akose muda wa kuwa na wewe pale anapokuhitaji, badala yake anaweza kwenda kwa mwanamke mwingine ambaye hayupo bize.

Thursday, July 6, 2017

Hii Ndio Mitego Ya Ma-House Girl Kwa Wanaume Wa Familia


Ndugu zangu, malalamiko ya baadhi ya mabinti wanaofanya kazi za ndani ‘mahausigeli’ kuwazidi kete baadhi ya wanawake kwa kuwachukulia waume zao yamekuwa yakiripotiwa kila mara.
Si ajabu hata wewe unayesoma makala haya aidha umeshawahi kumsikia rafiki kama siyo jirani yako akikorofishana na hausigeli wake au kushuhudia hausigeli akifumaniwa na bosi wake.

Hakika ni matukio ya aibu sana. Inafika wakati unajiuliza inakuwaje mume anamtongoza na hatimaye kutembea na hausigeli wake? Ameshawishiwa na kitu gani au amekosa nini kwa mkewe mpaka anafikia uamuzi huo?

Kimsingi linapotokea tukio kama hili, wengi hujiuliza maswali mengi sana na majibu yake huwa ni magumu kupatikana. Hii ni kwa sababu ni jambo lisilotarajiwa kufanywa na mtu aliyestaarabika. Hata hivyo, tuna kila sababu ya kujua chanzo cha tatizo hili.

Nitajaribu kuzungumzia kipengele kimoja baada ya kingine kuhusiana na yapi yanayotajwa kuwasukuma baadhi ya wanaume kutembea na mahausigeli wao.
Wanawake wanajitakia

Ni jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa sana na baadhi ya watu kuwa, inakuwaje hausigeli anapewa majukumu ya kumhudumia mume wakati mke yupo?

Ni ukweli usiofichika kwamba, kuna baadhi ya wanawake ni malimbukeni wasiojua jinsi ya kuitunza ndoa. Hawajui namna ya kumshika mume na kumuepusha na vishawishi vinavyoweza kumfanya akamsaliti.

Ndugu zangu, kitendo cha mke kumruhusu hausigeli amfulie mumewe nguo zake za ndani, amuandalie chakula, ampelekee maji ya kuoga na mambo mengine kama hayo ndivyo vimekuwa vikichochea usaliti huu.

Kama mke hataki kusalitiwa kirahisi basi ajitahidi sana kuchukua jukumu la kufanya yale ambayo kwa kiasi kikubwa yakifanywa na hausigeli huweza kujenga ukaribu wa kimapenzi kwa mumewe. Kamwe usibweteke, ukibweteka hausigeli wako atakupindua na itakuwa ni aibu kwako.
Mahausigeli micharuko

Hivi inaingiaje akilini mke kuridhia kumuajiri hausigeli ambaye kwa macho tu anaonekana hajatulia? Unamuajiri hausigeli ambaye siku ya kwanza tu anataka umpe sehemu ya mshahara wake akafanye ‘shopping’ halafu unakubali, unajitaka kweli?

Tuesday, July 4, 2017

Unayajua Madhara Ya Kuangalia Video za Ngono?...Je Unajua Namna Ya Kuacha?, Soma Hii Itakusaidia


Kuangalia video za ngono sio jambo jipya kwa jamii yetu, kimsingi ni watu wachache sana wanaweza kujizuia kujichua au kupiga punyeto baada ya kuangalia video za ngono.

Bahati mbaya tabia ya kuangalia video hizi watu wengi huipata wakiwa wadogo sana na usipokua makini tabia hii itakufanya vibaya sana kisaikolojia.

Tabia ya kujichua sasa iko wazi kwa jinsia zote yaani wanawake na wanaume japokua imekua ikiathiri zaidi wanaume sababu ya maumbile yao.

Japo wengi hufanya kwa siri na kuficha ili wasijulikane na wengine. Vijana wengi wamekuwa wakiangalia video hizo wakiwa wamejificha wenyewe chumbani, na hasa nyakati za usiku.
Kuangalia video za ngono kuna madhara mbalimbali ya kiafya na kisaikolojia. Haya hapa ni baadhi ya madhara unayoweza kuyapata kama utaangalia sana video za ngono.
Kuishiwa hamu ya tendo la ndoa na nguvu za kiume

Kuangalia sana video za ngono hukufanya ushindwe kusisimuliwa na mwanamke au mwanaume wa kawaida, video za ngono zina wanawake na wanaume wazuri sana ambao wako vile sababu ya kufanyiwa upasuaji mbalimbali wa kuongeza makalio na matiti, hata wanaume hufanyiwa upasuaji wa kuongeza uume hivyo mwanamke anayeangalia atatamani uume mkubwa kama ule au mwanaume anayeangalia atatamani mwanamke kama yule ambaye katika mazingira ya kawaida hayupo.

Sasa wanaume wanao angalia video za ngono hawawezi kusisimka au kuamsha uume hata mwanamke wa kawaida akipita uchi na hii huweza kuathiri sana mahusiano yao na kuonekana hawana nguvu za kiume kwani wao hutegemea video hizo kuamsha uume.

Kujichua au kupiga punyeto sana
Video za ngono zina wanawake na wanaume tofauti, kila video nzuri unayoangalia utaenda kujichua huku ukimuwaza wanaume au mwanamke husika. Hii itakufanya ujichue hata mara kumi kwa siku kama unaziangalia mara kwa mara. Kuishiwa nguvu za kiume, kusahau sana, kushindwa kumpa mwanamke mimba, kuchoka sana na kufika kileleni haraka wakati wa tendo la ndoa ni moja ya madhara makuu ya punyeto.

Kushindwa kudumu kwenye mahusiano
Kuangalia video za ngono hukufanya uwaze kujiridhisha mwenyewe tu na hata mwenza wako akitaka kulala na wewe unakua hutaki tena. Lakini hata kwa vijana ambao hawako kwenye mahusiano hujikuta wanakua waoga sana kuwafuata wanawake au wasione sababu ya kua kwenye mahusiano. Vile vile wanaume hushindwa kuwaridhisha wenza wao na wanawake kusingizia kuchoka kila siku.

Kuanza kufanya ngono ambazo sio za kawaida
Hivi karibuni idadi kubwa ya wanawake wamekua wakijihusisha sana na mapenzi ya kinyume na maumbile. Hii imesababishwa sana na kuangalia video za ngono na kuona ni kitu cha kawaida wakati kina madhara mengi. Wanawake waliozoea kuingiliwa nyuma hata wakiolewa huendelea kufanywa na wanaume wa nje hasa kama waume waliowaoa hawajawahi kujihusisha na tabia hiyo. Aina zingine za ngono ambazo zinababishwa na tabia ya kuangalia video hizi ni ushoga, usagaji, au mwanamke kulala na wanaume zaidi ya mmoja au mwanaume kulala na wanawake zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.

Inawezekana wewe unayesoma hapa tayari hii tabia inakuumiza sana kwa sasa na umeshindwa kuiacha, kuna mambo ya msingi unaweza kufanya ili uweze kuacha kuangalia video hizi..

Ondoa zana zote za kuangalia video hizi
Kama una tarakilishi (computer) au simu futa video zote, futa tovuti (website) zote za video ambazo unazitumia kuangalia. Kuna watu wamo kwenye makundi ya WhatsApp ya kutumiana video za ngono, ondoka kabisa huko kwani unajiharibu.

Anza kufanya mazoezi
Ni mazoezi pekee yanayoweza kumfanya mtu aweze kuachana na tabia zote ambazo sio za kawaida ambazo alikua anazifanya kipindi cha nyuma. Unapofanya mazoezi utatumia nguvu nyingi na mwili wako utachoka na kupata usingizi. Vilevile ufanyaji wa mazoezi hukuepusha na kukaa bila shughuli yoyote.

Jijengee tabia ya kukaa na marafiki zako muda mrefu au kufanya shughuli nyingine zitakazokuweka ‘busy’

Kama una tabia ya kuangalia video hizi basi, fanya mpango uwe unafanya mambo mengine muda ambao umekua ukiangalia hizi video, ikiwemo kusoma vitabu au kuongea na watu. Hii itakusaidia kusahau video hizo na kuacha kabisa.

Pata ushauri wa kitaalamu na matibabu
Unaweza kumuona mtaalamu wa ushauri wa kisaikolojia ili kukusaidia ushauri wa namna ya kufanya ili kuepukana na tabia hiyo. Kama umeshapata madhara kiafya, basi waone wataalamu wa afya hasa masuala ya uzazi ili wakushauri namna ya kulitibu tatizo lako.

Jenga mahusiano ya karibu na mpenzi wako
Hii itakusaidia kumuwaza yeye zaidi ya video za ngono na pia pale unapopata hamu ya kufanya mapenzi basi hutoogopa kumwambia ili mfanye. Kuwa karibu na mpenzi wako kutakujengea ujasiri na kuyakuza mahusiano yenu.

Njia Bora NNe Za Kumjua Asiyekuwa Na Penzi La Dhati Kwako!



Ifahamike kuwa hakuna asiyehitaji mapenzi ya kweli ingawa kuna wapenzi wanaothamini penzi wmenzi wake anapokuwa na pesa au kazi Fulani na baada ya hapo hujitoa katika mahusiano hayo hali ambayo huleta kwikwi katika mtima wa moyo wa anayefahamu kupenda.


I

1.      Muongo

Hakuna asiyefahamu athari za mtu muongo katika jamii, vivyo hivyo ndivyo ilivyo katika mapenzi uongo ni sumu mbaya na nidalili moja wapo ya kuonyesha kuwa mpenzi wako hana penzi la dhati nawe na huyo aweza kukuletea athari za kufikiri hapo baadae endapo hautakuwa makini nae. 

Hivi karibuni nilikuwa mjini Mbeya nikipata chakula katika moja ya mgahawa uliopo mkabala na Posta, katika mgahawa huo nilikutana na vijana wawili na msichana mmoja wakiwa wanakula chakula ambapo kati ya kijana mmoja alionekana kuwa ni mpenzi mpya wa yule binti ambaye alisikika akisema kiwa ‘’ukija kwangu atakalia sofa ambazo hujawahi kuziona maishani’’ hali iliyonishtua na kuelewa mara moja kati ya tabia alizonazo kijana yule ambaye anaonekana ni mcha Mungu.

Hivi utajisikiaje Mpenzi wako akigundua kuwa ulikuwa ukimdanganya na hatimaye yeye akajua ukweli wa suala ulilokuwa ukimpiga fiksi? Lakini ushauri wangu si kumacha bali jaribu kumshauri kwa hekima na akiendelea na tabia hiyo ujue kuwa hana mapenzi ya kweli kwako.

2.     Kupenda pesa

Ukiona mpenzi wako wa kike ama kiume anapenda sana kupata pesa kutoka kwako tambua ni moja ya dalili ambazo zinajieleza kuwa hana mpango nawe bali analazimika kuwa nawe kutokana na pesa ama kipato chako. Mpenzi wa namna hiyo ili kujihakikishia dalili hii siku moja akikuomba pesa hata kama ameziona mwambie kuwa huna, hapo yupo tayari kuvunja hata mahusiano kwasababu kitu muhimu kwake hajapata na wala wewe si muhimu tena kwake.

Nieleweke kuwa sisemi pesa ni mbaya katika mapenzi, la hasha bali pesa na mapenzi ni sawa na trafiki na kondakta katika mambo Fulani yale………ya kuchafua mifuko kwenye nguo nyeupe……………na ni muhimu wapenzi mkapenda kupeana maarifa ya kufanya kazi halali ili kujipatia vipato kwa ajili ya kuepukana na hili.

3.     Hajali kutokuwa jirani na wewe.

Mpenzi anaye kupenda muda mwingi hutamani kuwa nawe karibu na inapotokea hamjaonana hata masaa sita au matatu hujisikia shida ambapo kwa wengine hufikia kupiga simu na ukimuuliza anasemaje atakuuliza maswali yaliyoshonana kama ushanga mara upo wapi? Umekula? Na upo na nani? Na maswali mengi ya namna hiyo ili mradi moyo wake utulie.

Endapo Mpenzi wako mkiwa mbali naye kwa muda wa masaa mengi na yeye akaonyesha kuwa hakukosa chochote kutokuwa nawe karibu ama kuwasiliana nawe basi ujue kuwa mpenzi huyo ni kimeo yaani hana mapenzi ya dhati kwako.

4.     Anapenda kukuudhi

Dalili ya Nne ya mpenzi asiyekuwa na mapenzi ya dhati nawe ni yule anayependa kukuudhi mara kwa mara kana kwamba anatafuta sababu ya kuachana nawe lakini anashindwa kutamka bayana kuwa haitaji tena kuwa nawe.

Maudhi hayana budi kutokea pale inapobidi kwa bahati mbaya sana na si kwa makusudi, lakini wapo wapenzi wanaowaudhi wenzao kwa makusudi huku wakiendelea kusisitiza maudhi hayo kama utani na kujua kwa makusudi kuwa anamuumiza mwenzi wake bila kuomba msamaha. Ingawa kuomba msamaha ni kipaji na hasa katika mfumo dume ambao unaonesha kuwa mwanaume anapoomba msamaha basi ujue katumia njia nyingi za kumaliza tatizo hilo zimeshindikana hivyo kaomba msamaha kwa kulazimika sana na kwa siri.

Thursday, March 30, 2017

Namna ya kumfikisha kileleni kwa haraka na kwa ustadi mwanamke


Kuna njia mbalimbali za kumuongezea wigo mwanamke kufika kileleni na kuna kitu kimoja wanawake wote husema, "Kufika kileleni huitaji utulivu wa akili na hisia ".

Kama ukimweka mwanamke kwenye mazingira mazuri kiakili na kihisia, kuna uwezekano mkubwa na mwili wake kufuata na kumfanya afike kileleni.

Japo wanawake wanatofautiana, imejaribu kuongea na baadhi ya wanawake na wametumegea siri na kutupa njia nzuri ya kumfikisha kileleni mwanamke kwa haraka, japo ilikua mpaka tulipowapa baadhi ya siri zetu za kiume kidogo ndo wakalainika kutuambia...

Kama ukitaka kumfikisha kileleni kwa haraka, ni vizuri mwanamke ukamweka juu yako ili aweze kudhibiti kasi, msuguano na engo ya uume wako ndani yake, japo nawe unaweza kupata matamanio ya kumsaidia, ila ni vizuri ukamwacha mwenyewe ili usije kumharibia kasi anayoitaka yeye na kuitumia.

Inabidi upambane na matamanio yako na uendelee kutulia na umsikilize anataka wewe ukaeje ili ajiongezee msisimko zaidi na kwa sasa inabidi uutulize mwili huku mikono yako ikishughurika na uitumie vizuri, unaweza kuwa unampapasa sehemu za makalio yake au nyuma ya kichwa chake sehemu za shingoni mpaka kisogoni kwa hali ya kimahaba, na kama umekaa wima utajiongezea pointi zaidi kwa kumbusu shingoni na kuongea maneno mazuri ya kimahaba na kumsifia kwa uzuri wake na sifa nyingine

Kumtongoza MREMBO siyo kazi, Soma hapa namna ya kumtongoza na kumpata


Je , unamtamani msichana mrembo ambae kwa sasa ni kama marafiki ? au unavutiwa na yule demu unayemuona kila siku mtaani na unashidwa kujizuia sema hujui uanzaje ? Haijalishi kama unamjua au hamjuani , ila inapokuja kwenye kumtongoza mwanamke unachotakiwa kujua ni uelewa wa vitu kadhaa kuhusu jinsi kutamani kunavyokua na jinsi ya kufanyia kazi ili ufanikiwe .

Kumtongoza demu na vitu unavyotakiwa kujua

kwanza kabisa kama unataka kumtongoza msichana au kumfanya tu akupende tu , inabidi uwe mtu poa ambae anaweza kuvuta macho ya wasichana.

Kama hautaweza kua mtu anayeweza kumvutia msichana kirahisi , utakua bado unauwezo wa kumtongoza mwanamke unayempenda lakini itakua ngumu kuwezesha yeye akukubali .

Kiufupi fatisha njia hizi 11 rahisi na kiukweli kabisa utakua vizuri katika kutongoza na hata kwa mambo mengine yatakayofuata baada ya hapo.

Tumia njia hizi moja baada ya nyingine na ijapokua utacheza karata zako vizuri basi lazima umpate mrembo yoyote unayemtaka hata kama kuna watu wengine kibao wanamfukuzia .

1 . Kua karibu nae

Siku zote , kama unataka kumtokea msichana njia muhimu kabisa ni kuweza kumjua kwa undani .Usikurupuke kurupuke tu ukaanza kutongoza , msichana ataogopa au atakuona mtu rahisi kua nae na mwisho wa siku utaishia kumboa tu .

Ongea nae na upate kumjua vizuri . Mtumie message na usiwe na mzuka , mfanye awe kama rafiki kwanza . Usimtokee kwanza sema pia usisubiri sana maana ataanza kukuchukulia poa .

2 . Kua mtu unayependeka

Hii ni hatua muhimu sana . Na huu ndio wakati utagundua kama anahisia na wewe kweli au anakuchezea akili . Pia unapoongea nae mara kwa mara jaribu kugundua vitu anavyovipenda. Jaribu kuweka ukaribu nae kwenye kitu ambacho wote mnakipenda.

3 . Usilale Usiku

Ndio maana mitandao mingi ya simu ikawapa ofa za usiku watu kama nyie muongee usiku kucha . Usiku ndio muda sahihi wa kuweza kutoa ya moyoni na kueleza hisia zako kwa msichana . Anza kwa kuweka maongezi ya kawaida na kadiri unavyoendelea weka vionjo fulani vitakavyomfanya aanze kuingia line bila kugundua kama unamtokea.

4 . Ishi Maisha mawili

Unapoongea nae usiku , mwaga sera zako na funguka kuhusu mambo ya mapenzi sema mkikutana ana kwa ana mchana usiongelee mambo ya mapenzi kabisa labda aanze yeye na hivyo kumaanisha ashaingia line na anapenda maongezi hayo .

Pia epuka kuongelea kuhusu mambo yenu ya kimapenzi mnapokua na marafiki wengine bali fanyeni hivyo mkiwa wawili . Kwa kufanya hivyo unamfanya aamini kuna uhusiano motomoto wa siri unapikika kati yenu.

5 . Usimfanye ajue unampenda

Wanaume wengi ufanyaga kosa hili kubwa . Wanawaambia wanawake wanawapenda au wanahisia za kimapenzi kwao . Ni kweli unampenda , anajua hivyo tayari . Au hajui ? Unampigia simu kila saa , mnataniani kimapenzi na anaona uhusiano wenu kabisa .

Kwahiyo japokua anahisi unampenda , usije kuonyesha hivyo kwani anahitaji kusikia kutoka kwako ili ajihakikishia hisia zake . Chukulia poa na usifunguke kuhusu hisia zako kwake , kitendawili alichonacho ndicho kitamfanya azidi kukunata na kutaka kujua mwisho wa mambo .

Thursday, June 16, 2016

Utafiti unasema kuwa Picha za utupu hupunguza hamu ya kufanya mapenzi


Watoto wengi hupata njia ya kutazama picha za ngono mitandaoni wakiwa na umri mdogo, kwa mujibu wa utafiti.
Karibu asilimia 53 ya watoto walio kati ya umri wa miaka 11 na 16 wametizama picha za ngono mitandaoni, wote wakiwa ni asilimia 94, ya walioona picha hizo wakiwa na umri wa miaka 14 kulingana na utafiti wa chuo cha Middlesex.
Utafiti huo unasema kuwa vijana kama hao, wako kwenye hatari ya kupoteza hamu ya kushiriki mapenzi.
Serikali inasema kuwa ili kuhakikisha kuwa watoto wako salama na masuala ya mitandao ni jukumu kubwa.
Watafiti waliwahoji watoto 1,001 walio na umri kati ya miaka 11 na 16, na kugundua kuwa asilimia 65 ya wale walio na umri wa kati ya miaka 15-16, walikubali kuona picha za ngono sawa na asilimia 28 ya wale walio kati ya miaka 11 na 12.

Saturday, May 21, 2016

Michepuko na nyumba ndogo zina haya kwenye mapenzi


Hivi nini faida ya michepuko.,
hakuna cha mchepuko wa lami wala vumbi,mchepuko ni mchepuko tu.
Hutokuwa na amani ukiwa na mchepuko,utawaza kukamatwa tu masaa yote.
Ya nini presha aisee,kwanini usibaki njia kuu mbona maisha yanakuwa rahisi sana.Chagua unayempenda muweke na mfunze mwenza wako kuwa utakavyo..sasa kama wewe utakuwa unahangaika na kila chupi au wallet ipitayo tutaishi kweli.
kwanini uogopeshe ambao wanaingia kwenye ndoa waogope waone ni jela wanaingia,inaogopesha sana kama mnakaa baa mpaka saa kumi na una mke na familia au mume na watoto.
Kama unapenda kutoka kwanini usitoke na mwenza wako ,na kama hapendi basi toka ila wahi kurudi,usidhani hapendi unapokuwepo nyumbani hata kama ni mpiga kelele kiasi gani,bado anafurahia uwepo wako nyumbani.
tujifunze kuepusha baadhi ya magonjwa ya kujitakia,vifo vya bila kupangwa na mengineyo hatari

Mwanaume huhitaji nini kwenye mahusiano?



Mwanaume hujisikia kupendwa sana ikiwa mwanamke ataweza kumfanya ajisikie kuwa mtu mwenye uwezo na maarifa. Watafiti wa mahusiano wanakubaliana kwamba udhaifu wa asili wa mwanaume ni kutaka kutambuliwa. Ni kama hali fulani ya kutaka kujihakikishia kwamba anaweza. Maana yake ni kwamba anapoingia kwenye mahusiano, anategemea kuwa na mtu anaye appreciate uwezo wake. 

Anahitaji uutambue na kuukubali uwezo wake

Mwanaume anajisikia kupendwa sana ikiwa utaweza kumfanya ajisikie kuwa mtu mwenye uwezo na maarifa. Watafiti wa mahusiano wanakubaliana kwamba udhaifu wa asili wa mwanaume ni kutaka kutambuliwa. Ni kama hali fulani ya kutaka kujihakikishia kwamba anaweza. Maana yake ni kwamba anapoingia kwenye mahusiano, anategemea kuwa na mtu anaye appreciate uwezo wake.

Kama unatamani mwenzi wako wa kiume akupende, ni muhimu kujiuliza, "Hivi mume wangu ana uwezo gani... vipaji gani...ujuzi upi...anaweza nini ambacho wanaume wengine hawakiwezi...anasifika kwa lipi?" Ukishavibaini, mfanye ajue unavitambua vizuri. Mwambie asikie, utapandisha sana ego yake na atajiona kuwa mtu mwenye hadhi kwako kama mtu wake wa karibu na atajisikia kuchangamka moyoni.



Huenda unadhani hana uwezo mkubwa kivile, lakini ni lazima atakuwa na kitu anachokiweza. Huenda ni fundi mzuri na mwaminifu wa nguo. Pengine ni mtu asiyechelewa kurudi nyumbani atulie na familia yake. Labda hujituma kushiriki kazi za nyumbani na hata kuingia jikoni kukusaidia kukata kata nyanya. Huenda ni mwanasiasa maarufu au kiongozi mzuri kazini kwake. Au ni mtu mwaminifu na mfuatialiaji wa kila anachokiahidi na watu wanamwamini kwa hilo. Au pengine ni mcha Mungu anayeaminika kanisani. Au pengine ni mtangazaji hodari wa redio na televisheni. Chochote anachokifanya vizuri na unakijua, yakupasa kukitambua, na ukiseme kwa moyo wa dhati tena kwa kukirudia rudia, utamfanya ajiamini zaidi na kujaa nguvu za kupambana kufanya vizuri zaidi [anapenda kuwa hero wa mwenzi wake].

Mwanamke asiyeonyesha kutambua uwezo wa mume wake, tena akiwasifu wanaume wengine kwa yoyote wanayoyafanya, anatenda kosa la jinai. Hata kama unamsifu Baba Askofu, kuwa makini sana. Utaiporomoa ego yake vibaya sana, na huanza kujikuta akikosa hamu ya kuwa karibu na wewe [tutarejea hapa huko mbeleni]. Kwa hivyo kama ambavyo wewe huwezi kuchoka kuambiwa ulivyo mzuri, na yeye angependa kusikia alivyo na uwezo, kanuni ikiwa, mume wangu kwanza, wengine baadae. Maana, mwanaume humpenda mwanamke anayemfanya ajisikie mtu anayeweza, imara. hero na anayeaminika.

Anatamani anachofikiri kikubaliwe, sio kukosolewa

Kama kuna kitu kinaweza kumfanya mwanaume akakata tamaa na hata kuwa na hasira zisizoelewaka, basi ni kukosolewa, au kuambiwa anachotakiwa kufanya. Kukosolewa hushusha hadhi yake, na humfanya asijiamini na wakati mwingine ajihisi hana uwezo aliodhani anao. Hii ni hatari zaidi hasa kwa wanaume insecure. Unaweza kurejea suala hili hapa.

Hebu tuchukulie mwenzi wako amekuja na wazo la kufanya jambo fulani analodhani ni muhimu litekelezwe na nyie wawili kwa pamoja. Mwanamke mwenye uwezo wa kuchambua mambo, msomi, wakati mwingine anaweza akaona matatizo ya wazo lililoletwa. Asipoelewa hisia za mwanaume, mwanamke anayetaka kuamsha hasira za ndani, au za wazi za mwanaume, atamwambia moja kwa moja kuwa alichokifikiri hakina mashiko na KAMWE hawezi kukiunga mkono. Hii ni jinai.

Hata kama umeona mapungufu ya wazo lake, ni vizuri kwanza kutambua/appreciate na kuelewa umuhimu wa alichokisema yeye kwanza kisha, kwa hekima, chomeka wazo lako kama alternative route na sio kama wazo kuu linalofunika alichokipendekeza mwanaume. Ukiweza kufanya hivyo, utakuwa umelinda ego yake, na atajisikia salama kuwa na wewe.

Ndio maana utashangaa wanaume wengi wanapenda wanawake wasiosoma, wadogo kwa umri kwa sababu wanajua, hapatakuwa na 'ghasia za mijadala ya kibunge nyumbani'. Wanataka loyalty.  Lakini hata kama umesoma na unajiona huwezi kuburuzwa, jitahidi kushusha ego yako, mpe nafasi ajisikie 'kakutawala'! Shule inaweza kukukosesha mume hivi hivi ukienda na mawazo ya haki na fursa sawa kwa wote. Jifunze kushuka, na kumtanguliza mwanaume. Ndicho anachokitaka labda kama naye ana matatizo ya kulelewa kwenye familia ambayo mama ndiye aliyeoonekana kuongoza familia. Huyu utamwongoza, lakini kihisia sahau.

Kuungwa mkono ni pamoja na pale inapotokea mmepishana. Mwanaume kwa asili angetamani, hata kama amekosea yeye, uwe na uwezo wa kushuka na kuomba msamaha. Ndio gharama ya kuingia kwenye mahusiano. Kama una bahati na yeye mwenyewe ameweza kupambana na ego yake kiasi cha kutosha kuomba msamaha kumaliza ugomvi, mshukuru Mungu. Lakini kama mwanamke, unawajibu wa kuwa mjanja kubeba mzigo. Kama kuna haja ya kujadili suala hilo unaloamini amekosea yeye, tafuta wakati mwingine mnapokuwa katika hali ya kawaida, kisha msaidie kulitazama suala hilo more objectively. Atakuelewa.

Anahitaji kuheshimiwa

Heshima ya mwanamke kwa mwanaume inajionyesha si tu kupitia maneno anayoyasema bali hata kwa lugha ya mwili kama macho na mdomo. Na huwezi kuamini, wanaume wengi wako very sensitive kupima namna unavyoonyesha heshima yako kwake.

Jiulize kama mwanamke, huwa unaongeaje na mumeo hasa anapokukosea? Unapandisha sauti juu? Unambetulia mdomo? Unajaribu mara zote kumfanya afuate unachokitaka wewe? Unamwelekeza cha kufanya? Unajenga picha ya kumwona kama mtu asiyeweza kwenda ibadani bila kuambiwa? [he he, hapa ni kazi, twende kwa tahadhari]. Unaonyesha kuwa unaweza kuishi bila kipato chake? Unaonyesha kutokumwamini na kumhisi hisi? Unamchapa jicho la 'dharau' mkiwa wawili au mbele za watu, tena wakati mwingine mbele za watu wanaomheshimu? Mara nyingi, unaweza usiseme, lakini kama mwili wako, maneno yako au matendo yako yakatuma ujumbe, "Hivi wewe mbona umefanya ujinga hivi?" na hapo, utakuwa umeamua kurarua ego, hadhi yake. Matokeo yake, kuna mpole tutayaona kwenye makala zinazofuata.

Heshima, maana yake ni kuhakikisha mwanaume unayempenda hajisikii 'kufanywa mtoto mdogo' asiyeweza kufanya lolote bila mwongozo 'wa kitaalam' wa mke wake. Kwa mfano, unapokuwa mtu wa kutoa maelekezo yasiyoisha kwa mumeo, "fanya hivi...nakuambiaga siku zote...halafu ukumbuke kufanya kile... usisahau lile na lile... uende kule tulikokubaliana kwa wakati... ", maana yake unamwambia hana uwezo wa kufanya majukumu yake bila maelekezo yako. Anakuona arrogant. Hapo akiendelea na wewe kwa amani, amekuvumilia, au basi yuko down to earth.

Usijaribu kumfanya mwanaume akuone kama toleo la pili la mama yake. Akikuona una-behave kimama mama, ataanza kujisikia ukilaza fulani ndani yake, na hatimaye atajikuta anatafuta uhuru wake. His space. Namna fulani ya kujiweka mbali na wewe. Ukisema anakuitikia, ila hafanyi.

Chukulia umekutana na mchumba wako, na umegundua shati alilovaa haliendani kwa vyovyote vile na suruali yake au hajanyoa ndevu kabisa, na zinakukera. Kuona hivyo, na kwa jinsi unavyotaka uonekaneclassic ukiwa nae,  bila kusita unarushia swali ambalo kimsingi ni maoni, "Darling, hukujitazama kwenye kioo ulipondoka nyumbani?...hilo shati vipi tena mwenzagu?"

Au umeenda nyumbani kwake, ukakuta viatu vimewekwa bila utaratibu, nawe, kama kawaida yako, unaanza mambo yako, tena kwa tone ya utani hivi,"Hubby, sipendi kabisa nikikuta sebule iko rough hivi?", wakati huo, unavikusanya na kuviweka mahali pake. Ingawa ni kweli umechangia kueleta mwonekano chanya kwenye sebule yake/yenu, umetumia lugha gani? Umeonyesha tatizo, ili ujikweze kwamba unaelewa zaidi?

Sasa ni vizuri kujiuliza mwenyewe, je, unatambua uwezo wa mpenzi wako hata pale ambapo amekosea wazi? Unamshauri kwa lugha inayoonyesha kuboresha alichonacho, au unajenga picha ya mtu anayejifanya anajua kila kitu (bi'haambiliki)? Kwa sababu, mwisho wa siku, heshima kwa mwanume ni kuamini uwezo wake, kumfanya ajione anaweza kutekeleza majukumu bila 'consultancy' ambayo hajaiomba. Huo ndio upendo katika lugha ya mwanaume. Fanya kinyume, shughuli yake utaiona.

Wewe sio mwaminifu kwa mpenzi wako?, umejiuliza kwanini....!!!?


Hapa nazungumza na wale ambao wanatamani kuwa waaminifu kwa wapenzi wao. Yapo mambo mengi, lakini hapa ninajitahidi kueleza yale ya muhimu zaidi. Wiki iliyopita niliishia kwenye kipengele cha mitandao ya kijamii, kwa kuwa sikukimaliza, tutaendelea hapo.MITANDAO YA KIJAMII
Utafiti usio rasmi unaonesha kwamba, pamoja na kwamba mitandao ya kijamii imesaidia kwa kiasi kikubwa sana kurahisisha upatikanaji wa taarifa, kuendesha mijadala na kukuza ufahamu wa mambo mengi, suala la mapenzi limetajwa!

Utakutana na mtu Facebook (mfano), mmekuwa marafiki, lakini siku ya siku anaanzisha mambo ya mapenzi. Kwa sababu umeshakuwa naye karibu kwa muda mrefu, umekuwa wazi kwake ni rahisi kuanguka!
Hisia za mapenzi wakati mwingine hudanganya. Ngoja niwaambie ukweli, unapokuwa unawasiliana sana na mtu wa jinsi tofauti na yako, hisia za mapenzi huwa kali sana, kiasi kwamba ukiambiwa tu unapendwa, ni rahisi kuingia mkenge!

Kwenye mitandao ya kijamii kwa mfano Facebook, BBM, Twitter na mingineyo maarufu kuna utamaduni wa kuweka picha. Wakati mwingine picha hudanganya...kwa haraka haraka mtu eti anasema amekupenda. Hakuna lolote zaidi ya kuwaza ngono tu!
Huo ndiyo ukweli. Tatizo ni kwamba, huwezi kujua kama kuna hatari hiyo mbele yako. Unao marafiki wengi, mnataniana kila wakati, siku akilianzisha, inakuwa ngumu kuchomoka. Hata hivyo, kuna mambo madogo sana ukiyafanya yatasaidia kukutoa kwenye mtego.
Utakuta mtu ana mpenzi wake, mke au mume. Kifupi yupo kwenye uhusiano, lakini kwenye mtandao anaandika yupo ‘single’. Kwa nini hutaki kujulikana kuwa upo kwenye uhusiano?
Hujiamini? Humpendi mpenzi wako au tatizo ni nini hasa? Rafiki zako wanapoona huna mtu kwenye maelezo yako, wanatumia nafasi hiyo kukutega. Kwa nini ujiweke kwenye mitego? Kama upo kwenye uhusiano, kuwa mkweli, andika.
Ikiwezekana sehemu ya kuweka picha yako, weka ya mpenzi wako au mliyopiga pamoja, hii itasaidia marafiki kukuheshimu na wale wenye tabia za kipuuzi kujitoa mapema.
Wanaotumia mitandao ya kijamii ni mashahidi wa hiki ninachokizungumzia hapa.

MAVAZI
Kipengele hiki kinawagusa zaidi wanawake. Mavazi yanazungumza! Ulivyovaa ndivyo unavyojitafsirisha kwa wanaokutazama. Inawezekana ukawa ni mwaminifu kwa mwenzako na unajitahidi sana kuhakikisha unakuwa katika hali hiyo, lakini mavazi yako yanaweza kukutibulia.

Kwa nini uvae nguo zinazoonesha maungo yako ya ndani? Mchumba au mke wa mtu, kwa nini uvae vinguo vya ovyo? Unamwonesha nani sasa huko barabarani? Ndugu zangu, sijawahi kuona mwanamke aliyevaa kiheshima akapata usumbufu kwa wanaume njiani.
Hata kama unajijua huwezi kutegeka, lakini nataka kukuhakikishia kwamba, kusumbuliwa sana ni njia ya kuelekea kwenye usaliti. Ipo mifano hai; Kuna dada mmoja alikuwa anavaa vinguo vya kubana, kila akipita anasumbuliwa na mwanaume fulani hivi mtaani kwao.

Ameshamtumia watu mara nyingi, lakini anakataa. Siku moja ikatokea amehitilafiana na mpenzi wake, kwa hasira akaamini kuwa ameshaachana naye na hamtaki tena. Alipopita ile sehemu, yule jamaa akamuita.
Akilini mwake, akaona hakuna sababu ya kumtesa yule jamaa wakati amegombana na mpenzi wake. Kwa lengo la kujiliwaza akaenda, jamaa alilala naye siku hiyo hiyo! Alijuta baada ya kumaliza tendo!
Ya nini yote hayo? Vaa mavazi ya heshima. Jisogeze kwenye uaminifu. Ni nani atakayekusumbua ikiwa mavazi yako yanaonesha heshima uliyonayo?
Usikose wiki ijayo katika sehemu ya mwisho, kuna mambo mengi ya muhimu unayotakiwa kujua.

Tuesday, April 19, 2016

Kwa wanume, haya ni mazoezi yanayoongeza nguvu za kiume!

Mwanaume kikawaida unatakiwa mwili wako uwe umechangamka sana kwa mazoezi ya hapa na pale lakini utakuta mwanaume anapata muda wa kukaa kwa dakika tisini au zaidi akiangalia mpira, au masaa manne, matano na wengine wanakesha kabisa katika baa wakinywa na kula tu
, lakini wanasahau kabisa kutenga muda tena mdogo tu kama dakika tano mpaka nane kwa siku kwa ajili ya kuimarisha nguvu za kiume kwa kufanya mazoezi ya kuongeza nguvu za kiume.

Mwanaume anefanya mazoezi ya kuimarisha misuli ya uume hawezi kuwa sawa na mwanaume asiyefanya mazoezi haya sio tu katika kuimarisha nguvu zake za kiume lakini pia kuweza kujitawala katika tendo la ndoa na kuweza kumfikisha mwanamke katika raha ile inayotakiwa.
Mazoezi  haya yakifanywa kwa dhati yanaweza kumpa mtu matokeo mazuri sana ilimradi afuate utaratibu atakao takiwa aufuate.
Hizi ni miongoni mwa faida zinazopatikana kwa kufanya mazoezi haya ni hizi zifuatazo:
Kwanza humpa uwezo mwanaume kuweza kusimamisha uume wake kwa muda mrefu zaidi kuliko ambavyo alikuwa anaweza kuusimamisha  kabla ya kufanya mazoezi haya.
Pili mazoezi haya hufanya mtiririko wa damu kwenye uume uwe mzuri hivyo kuufanya uume uwe na nguvu na kuondoa kabisa tatizo la nguvu za kiume.
Tatu humpa uwezo mfanyaji wa mazoezi haya kukawia kumwaga mbegu hivyo kumpa nafasi mwanamke aweze kufikia katika kilele chake pasi na kumkatishia njiani.

Vifaa Unavyohitaji
1.   Mafuta ya mizeituni (Olive Oil) au mafuta ya nazi au Alizeti au mafuta ya mgando (gel)
2.   Jiko  lolote ili upate mvuke wa kutosha unaweza kutumia jiko la mchina, stove, au hata la mkaa lakini isiwe moto mwingi uwe kiasi tu lengo ni mvuke
3.   Kitambaa kisafi na laini na maji safi ya uvuguvugu

Namna ya kufanya mazoezi ya Kuongeza nguvu za kiume
1. Loweka kitambaa chako katika maji ya uvugu vugu kisha anza kwa kuusafisha uume wako kwa kitambaa laini cheye maji ya uvugu vugu kama unauchua uume kwa kuuvuta mbele. Fanya zoezi hili kwa dakika tatu.

2.  Pakaa mafuta yako kwenye viganja vyako viwili vya mikono yako kama vile unataka kujipaka mafuta mwilini.

3.  Weka viganja vyako ili vipate mvuke wa moto kutoka katika ama jiko la mchina, stove au kitu chochote utakachotumia. Ukiona viganja vimepata joto kiasi cha kutosha siyo mpaka uungue mikono, kisha

4.  Kamata uume wako ukiwa unauchua kwa kuuvuta mbele kwa nguvu kidogo sana ukianza na mkono wa kulia alafu wa kushoto au kushoto halafu kulia vile utakavyoona inafaa. Joto kwenye mikono likiisha rudisha mikono yako uipashe tena ili ipate joto kisha rudia  kuuvuta vuta tena uume kwa muda wa dakika kumi.

Kumbuka
Mazoezi haya hufanywa mara mbili asubuhi tu mtu ukiamka na wakati ukitaka kwenda kulala na ni kwa muda wa wiki tatu. Utaona matokeo yake.