Mwanaume hujisikia kupendwa sana ikiwa mwanamke ataweza kumfanya ajisikie kuwa mtu mwenye uwezo na maarifa. Watafiti wa mahusiano wanakubaliana kwamba udhaifu wa asili wa mwanaume ni kutaka kutambuliwa. Ni kama hali fulani ya kutaka kujihakikishia kwamba anaweza. Maana yake ni kwamba anapoingia kwenye mahusiano, anategemea kuwa na mtu anaye appreciate uwezo wake.
Anahitaji uutambue na kuukubali uwezo wake
Mwanaume anajisikia kupendwa sana ikiwa utaweza kumfanya ajisikie kuwa mtu mwenye uwezo na maarifa. Watafiti wa mahusiano wanakubaliana kwamba udhaifu wa asili wa mwanaume ni kutaka kutambuliwa. Ni kama hali fulani ya kutaka kujihakikishia kwamba anaweza. Maana yake ni kwamba anapoingia kwenye mahusiano, anategemea kuwa na mtu anaye appreciate uwezo wake.
Kama unatamani mwenzi wako wa kiume akupende, ni muhimu kujiuliza, "Hivi mume wangu ana uwezo gani... vipaji gani...ujuzi upi...anaweza nini ambacho wanaume wengine hawakiwezi...anasifika kwa lipi?" Ukishavibaini, mfanye ajue unavitambua vizuri. Mwambie asikie, utapandisha sana ego yake na atajiona kuwa mtu mwenye hadhi kwako kama mtu wake wa karibu na atajisikia kuchangamka moyoni.
Huenda unadhani hana uwezo mkubwa kivile, lakini ni lazima atakuwa na kitu anachokiweza. Huenda ni fundi mzuri na mwaminifu wa nguo. Pengine ni mtu asiyechelewa kurudi nyumbani atulie na familia yake. Labda hujituma kushiriki kazi za nyumbani na hata kuingia jikoni kukusaidia kukata kata nyanya. Huenda ni mwanasiasa maarufu au kiongozi mzuri kazini kwake. Au ni mtu mwaminifu na mfuatialiaji wa kila anachokiahidi na watu wanamwamini kwa hilo. Au pengine ni mcha Mungu anayeaminika kanisani. Au pengine ni mtangazaji hodari wa redio na televisheni. Chochote anachokifanya vizuri na unakijua, yakupasa kukitambua, na ukiseme kwa moyo wa dhati tena kwa kukirudia rudia, utamfanya ajiamini zaidi na kujaa nguvu za kupambana kufanya vizuri zaidi [anapenda kuwa hero wa mwenzi wake].
Mwanamke asiyeonyesha kutambua uwezo wa mume wake, tena akiwasifu wanaume wengine kwa yoyote wanayoyafanya, anatenda kosa la jinai. Hata kama unamsifu Baba Askofu, kuwa makini sana. Utaiporomoa ego yake vibaya sana, na huanza kujikuta akikosa hamu ya kuwa karibu na wewe [tutarejea hapa huko mbeleni]. Kwa hivyo kama ambavyo wewe huwezi kuchoka kuambiwa ulivyo mzuri, na yeye angependa kusikia alivyo na uwezo, kanuni ikiwa, mume wangu kwanza, wengine baadae. Maana, mwanaume humpenda mwanamke anayemfanya ajisikie mtu anayeweza, imara. hero na anayeaminika.
Anatamani anachofikiri kikubaliwe, sio kukosolewa
Kama kuna kitu kinaweza kumfanya mwanaume akakata tamaa na hata kuwa na hasira zisizoelewaka, basi ni kukosolewa, au kuambiwa anachotakiwa kufanya. Kukosolewa hushusha hadhi yake, na humfanya asijiamini na wakati mwingine ajihisi hana uwezo aliodhani anao. Hii ni hatari zaidi hasa kwa wanaume insecure. Unaweza kurejea suala hili hapa.
Hebu tuchukulie mwenzi wako amekuja na wazo la kufanya jambo fulani analodhani ni muhimu litekelezwe na nyie wawili kwa pamoja. Mwanamke mwenye uwezo wa kuchambua mambo, msomi, wakati mwingine anaweza akaona matatizo ya wazo lililoletwa. Asipoelewa hisia za mwanaume, mwanamke anayetaka kuamsha hasira za ndani, au za wazi za mwanaume, atamwambia moja kwa moja kuwa alichokifikiri hakina mashiko na KAMWE hawezi kukiunga mkono. Hii ni jinai.
Hata kama umeona mapungufu ya wazo lake, ni vizuri kwanza kutambua/appreciate na kuelewa umuhimu wa alichokisema yeye kwanza kisha, kwa hekima, chomeka wazo lako kama alternative route na sio kama wazo kuu linalofunika alichokipendekeza mwanaume. Ukiweza kufanya hivyo, utakuwa umelinda ego yake, na atajisikia salama kuwa na wewe.
Ndio maana utashangaa wanaume wengi wanapenda wanawake wasiosoma, wadogo kwa umri kwa sababu wanajua, hapatakuwa na 'ghasia za mijadala ya kibunge nyumbani'. Wanataka loyalty. Lakini hata kama umesoma na unajiona huwezi kuburuzwa, jitahidi kushusha ego yako, mpe nafasi ajisikie 'kakutawala'! Shule inaweza kukukosesha mume hivi hivi ukienda na mawazo ya haki na fursa sawa kwa wote. Jifunze kushuka, na kumtanguliza mwanaume. Ndicho anachokitaka labda kama naye ana matatizo ya kulelewa kwenye familia ambayo mama ndiye aliyeoonekana kuongoza familia. Huyu utamwongoza, lakini kihisia sahau.
Kuungwa mkono ni pamoja na pale inapotokea mmepishana. Mwanaume kwa asili angetamani, hata kama amekosea yeye, uwe na uwezo wa kushuka na kuomba msamaha. Ndio gharama ya kuingia kwenye mahusiano. Kama una bahati na yeye mwenyewe ameweza kupambana na ego yake kiasi cha kutosha kuomba msamaha kumaliza ugomvi, mshukuru Mungu. Lakini kama mwanamke, unawajibu wa kuwa mjanja kubeba mzigo. Kama kuna haja ya kujadili suala hilo unaloamini amekosea yeye, tafuta wakati mwingine mnapokuwa katika hali ya kawaida, kisha msaidie kulitazama suala hilo more objectively. Atakuelewa.
Anahitaji kuheshimiwa
Heshima ya mwanamke kwa mwanaume inajionyesha si tu kupitia maneno anayoyasema bali hata kwa lugha ya mwili kama macho na mdomo. Na huwezi kuamini, wanaume wengi wako very sensitive kupima namna unavyoonyesha heshima yako kwake.
Jiulize kama mwanamke, huwa unaongeaje na mumeo hasa anapokukosea? Unapandisha sauti juu? Unambetulia mdomo? Unajaribu mara zote kumfanya afuate unachokitaka wewe? Unamwelekeza cha kufanya? Unajenga picha ya kumwona kama mtu asiyeweza kwenda ibadani bila kuambiwa? [he he, hapa ni kazi, twende kwa tahadhari]. Unaonyesha kuwa unaweza kuishi bila kipato chake? Unaonyesha kutokumwamini na kumhisi hisi? Unamchapa jicho la 'dharau' mkiwa wawili au mbele za watu, tena wakati mwingine mbele za watu wanaomheshimu? Mara nyingi, unaweza usiseme, lakini kama mwili wako, maneno yako au matendo yako yakatuma ujumbe, "Hivi wewe mbona umefanya ujinga hivi?" na hapo, utakuwa umeamua kurarua ego, hadhi yake. Matokeo yake, kuna mpole tutayaona kwenye makala zinazofuata.
Heshima, maana yake ni kuhakikisha mwanaume unayempenda hajisikii 'kufanywa mtoto mdogo' asiyeweza kufanya lolote bila mwongozo 'wa kitaalam' wa mke wake. Kwa mfano, unapokuwa mtu wa kutoa maelekezo yasiyoisha kwa mumeo, "fanya hivi...nakuambiaga siku zote...halafu ukumbuke kufanya kile... usisahau lile na lile... uende kule tulikokubaliana kwa wakati... ", maana yake unamwambia hana uwezo wa kufanya majukumu yake bila maelekezo yako. Anakuona arrogant. Hapo akiendelea na wewe kwa amani, amekuvumilia, au basi yuko down to earth.
Usijaribu kumfanya mwanaume akuone kama toleo la pili la mama yake. Akikuona una-behave kimama mama, ataanza kujisikia ukilaza fulani ndani yake, na hatimaye atajikuta anatafuta uhuru wake. His space. Namna fulani ya kujiweka mbali na wewe. Ukisema anakuitikia, ila hafanyi.
Chukulia umekutana na mchumba wako, na umegundua shati alilovaa haliendani kwa vyovyote vile na suruali yake au hajanyoa ndevu kabisa, na zinakukera. Kuona hivyo, na kwa jinsi unavyotaka uonekaneclassic ukiwa nae, bila kusita unarushia swali ambalo kimsingi ni maoni, "Darling, hukujitazama kwenye kioo ulipondoka nyumbani?...hilo shati vipi tena mwenzagu?"
Au umeenda nyumbani kwake, ukakuta viatu vimewekwa bila utaratibu, nawe, kama kawaida yako, unaanza mambo yako, tena kwa tone ya utani hivi,"Hubby, sipendi kabisa nikikuta sebule iko rough hivi?", wakati huo, unavikusanya na kuviweka mahali pake. Ingawa ni kweli umechangia kueleta mwonekano chanya kwenye sebule yake/yenu, umetumia lugha gani? Umeonyesha tatizo, ili ujikweze kwamba unaelewa zaidi?
Sasa ni vizuri kujiuliza mwenyewe, je, unatambua uwezo wa mpenzi wako hata pale ambapo amekosea wazi? Unamshauri kwa lugha inayoonyesha kuboresha alichonacho, au unajenga picha ya mtu anayejifanya anajua kila kitu (bi'haambiliki)? Kwa sababu, mwisho wa siku, heshima kwa mwanume ni kuamini uwezo wake, kumfanya ajione anaweza kutekeleza majukumu bila 'consultancy' ambayo hajaiomba. Huo ndio upendo katika lugha ya mwanaume. Fanya kinyume, shughuli yake utaiona.
No comments:
Post a Comment