Latest News

Showing posts with label Maajabu. Show all posts
Showing posts with label Maajabu. Show all posts

Tuesday, June 6, 2017

Nabii Wa Ajabu Aonekana Kwa TB Joshua!


Nabii alisababisha utata nchini Afrika Kusini, mwaka 2015, baada ya kuwafanya waumini wake kula nyoka, panya na nywele ameonekana kwenye ibada nchini Nigeria ya muhubiri maalufu TB Joshua.

Muhubiri Penuel Mnguni ameoneaka katika ibada iliyoongozwa na mhubiri TB Joshua katika kanisa lake na aliweza kutoa ushuhuda umaosema kuwa ”nilianza kutizama TV za Emmanuel TV na kumsikiliza nabii TB Joshua, nikafahamu kuwa nilichokuwa nikifanya haikiendani na maandiko. Na nilivyofahamu kuwa lilikuwa shambulio nikaja hadi kwa TB Joshua ili anikomboe.”

Kupitia akaunti yake ya twitter Muhubiri Joshua aliweza kutwit kwa kuonesha kuwa alimpokea mchungaji huyo katika kanisa lake.
Nabii Mngui amebadilisha moyo wake, kwa mujibu wa gazeti la Citizen baada ya kujikuta akiandamwa mara kwa mara na kupelekea kushtakiwa na chama cha kupambana na dhuluma dhini ya wanyama (Society for the Prevention of Cruelty to Animals) Afrika Kusini, hata hivyo mastaka hayo yalifutwa mwaka 2015 Julai baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha.

Monday, May 15, 2017

Bibi kizee apandishwa kizimbani akidaiwa kuiba gari

Katika habari za kushangaza Tanzania basi hii inaweza kuwa mojawapo. 

Fatuma Mohammed (70) na Aziz Njakula (36) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya wizi na kupatikana na gari la wizi aina ya Toyota Hiace.
Wakili wa Serikali, Hamisi Said amedai leo (Jumatatu) mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa Julai 9, 2015 eneo la Mnazi Mmoja walitenda kosa la wizi wa gari hilo mali ya kampuni ya Choice Motors.
Januari 26, 2016 eneo la Nzasa, Dar es Salaam Mohammed anadaiwa alikutwa akiwa na gari la wizi nyumbani kwake.
Baada ya kusomewa mashtaka washtakiwa wamekana na upande wa Jamhuri ulidai upelelezi haujakamilika.
Hakimu Simba ametoa masharti ya dhamana kwamba wawe na wadhamini wawili kila mmoja ambao watasaini bondi ya Sh10 milioni. Walikamilisha masharti na kuachiwa kwa dhamana.

Source: Mwananchi

Wednesday, April 5, 2017

AUDIO: Amuua Mpenzi Wake Na Kuweka Maiti Kwenye Jaba


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema

 limemkamata mtuhumiwa Musuguri David (29) anayedaiwa

 kumuua mpenzi wake Samira Masoud (34) kwa kumchinja

 kisha mwili wake kuwekwa katika jaba la maji kisa wivu wa

 mapenzi maeneo ya Kibamba.

Thursday, March 30, 2017

AUDIO: MAPEPO YAVAMIA WANAFUNZI SHULE YA IMESELA SHINYANGA VIJIJINI,SHUHUDIA HAPA YAKIWATESA MBELE YA MKUU WA WILAYA


Ushirikina!! Ndivyo unavyoweza kusema…Wanafunzi wa shule ya sekondari Imesela iliyopo kata ya Imesela wilaya ya Shinyanga(Shinyanga vijijini) mkoa wa Shinyanga wamekumbwa na mapepo yanayowafanya waanguke na kupiga kelele wakitamka maneno yasiyoeleweka huku wakiwataja baadhi ya watu wanaofanya ushirikina huo.

Tatizo la wanafunzi wa kike kuanguka na kupiga kelele shuleni hapo lilianza mwezi Januari mwaka huu lakini hali hiyo ilikithiri Machi 20 mwaka huu ambapo wanafunzi takribani 16 wakianguka na kuanza kutamka maneno wakiwataja baadhi ya watu wanaofanya ushirikina shuleni hapo. 

Wanafunzi hao wamekuwa wakiugua ugonjwa usiojulikana wa kuanguka na kupoteza fahamu na kutamka maneno yasiyoeleweka kitendo ambacho kinahusishwana imani za kishirikina.

Inaelezwa kuwa mapepo hayo huwasumbua hasa wanafunzi wa kike mara tu wanapofika shuleni majira ya saa moja na nusu asubuhi mpaka saa tano lakini pia kuanzia saa saba mchana mpaka saa tisa alasiri wanapotawanyika kurudi majumbani mwao.

Aidha inadaiwa kuwa wanafunzi hao mara tu wanapopatwa na mapepo hayo huanguka na kupiga kelele huku wakigaragara na kuwarushia ngumi wanafunzi wenzao.
Shule ya sekondari Imesela iliyoanzishwa mwaka 2006 ina jumla ya wanafunzi 252 kati yao 130 ni wa kike na 122 ni wa kiume huku walimu wa wakiwa 14 ambapo mmoja pekee ni mwanamke.
Walimu wa shule hiyo wanasema vitendo hivyo vya kishirikina vinaathiri utaratibu wa vipindi vya wanafunzi hao ambapo wamekuwa wakitumia muda mwingi kusaidiana na wanafunzi wa shule hiyo kuwasaidia wanafunzi wanaopatwa na majanga hayo.
Mkuu wa shule hiyo Seleman Kalavina amesema mauza uza huanza kila siku asubuhi pindi tu wanapofika shuleni hali inayowafanya wanafunzi kupoteza muda wao wa masomo huku ikiwakatisha tamaa walimu wa shule hiyo kufundisha na kutamani kuhama shule hiyo.
Mratibu wa Elimu kata ya Imesela Julius Wamba amesema wamefanya jitihada za kuwaita viongozi wa dini kufika shuleni na kufanya maombi ili kumaliza tatizo hilo lakini mara tu wanapoondoka tatizo hujirudia. 

Kutokana na mauza uza hayo,leo Jumatano Machi 29,2017 mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama amelazimika kufika katika shule hiyo na mara baada tu ya kufika mashetani yakawapanda wanafunzi hao. 

Mkuu huyo wa wilaya amelazimika kuifunga shule hiyo kwa muda siku mbili ili viongozi na wananchi wa eneo hilo wakutane naye siku ya Ijumaa wiki hii ili kujadili namna ya kumaliza tatizo hilo. 

“Serikali haiamini ushirikina,hivi vitendo mnavyofanya siyo vizuri,watoto wanashindwa kusoma kwa sababu ya ushirikina wenu,tena mnawatesa watoto wa kike tu,hamtaki wasome mnataka kuwaoa? Si mkarogane wenyewe muwaache watoto wasome,nataka siku ya Ijumaa wote tukutane hapa tujadili namna ya kuw
asaidia wanafunzi hawa”,alisema Matiro. 

Malunde1 bog imeshuhudia wanafunzi hao wakianguka ovyo na kutamka maneno ya ajabu ajabu huku wengine wakitaka kupigana mpaka pale wanafunzi wenzao wanapoamua kuwakamata na kuwafunga na nguo mikononi na miguuni ili wasikimbie kisha kuanza kuwafanyia maombi.

Source: Malunde

Sunday, February 19, 2017

Maajabu: Manati yanayotumika kurudha dawa za kulevya yagunduliwa!


Maafisa wa Marekani wanaoshika doria mpakani, wamegundua manati kubwa ambayo ilikuwa imefungamanishwa na ua ulio kwenye mpaka wa taifa hilo na Mexico.
Manati hiyo inaonekana kuundwa mahsusi kwa ajili ya kurusha dawa za kulevya hadi Marekani.
Marekani imekuwa ikikabiliana sana na walanguzi wa mihadarati kutoka Mexico pamoja na wahamiaji.
Rais Donald Trump ameahidi kujenga ukuta mrefu sana kuzuia hilo.
Manati hiyo kubwa iligunduliwa na maafisa kusini mashariki mwa Tucson, Arizona, wiki iliyopita.
Wanasema waliwaona wanaume kadha wakitawanyika na kutoroka walipogundua kwamba maafisa hao walikuwa wanafika.
Maafisa hao walipokagua eneo hilo, waligundua vifurushi viwili vya bangi, vilivyokuwa na bangi ya jumla ya kilo 21.
Vifurushi hivyo vilikuwa bado havijarushwa.
Manati hiyo ambayo ilikuwa imejengwa upande wa Mexico wa ua ilibomolewa.
Hakuna aliyekamatwa kuhusiana na kisa hicho.
Takriban umbali wa maili 650 kati ya maili 1,100 (1,770km) za mpaka wa Mexico na Marekani tayari kumejengwa ua au ukuta.
Trump ameahidi kujenga ukuta mrefu lakini walanguzi wamekuwa wakitumia ubunifu katika kutumia njia za kufikisha madawa Marekani.
Miongoni mwa njia hizi ni kutumia ndege ndogo zisizo na marubani na wakati mwingine kuchimba njia za chini kwa chini zinazofika hadi Marekani.
Mwezi Machi, maafisa waligundua njia ya chini kwa chini ya umbali wa mita 380 ambayo ilikuwa imetoka kwenye mgahawa mmoja Mexico hadi kwenye jumba moja California.

Friday, January 27, 2017

Jicho la mchezaji latoka akiwa uwanjani

Mchezaji wa mpira wa kikapu nchini New Zealand Akil Mitchell amesema anapata nafuu baada ya jicho lake kutoka alipokuwa uwanjani akicheza.
Mitchell huchezea klabu ya New Zealand Breakers, na alikuwa mjini Auckland kucheza mechi ya NBL ya Australia Alhamisi usiku kisa hicho kilipotokea.
Mchezaji wa timu pinzani aliingiza kimakosa kidole ndani ya tundu la kishimo cha jicho na ghafla jicho lake likatoka nje.
Mchezaji huyo mzaliwa wa Marekani alianguka sakafuni akiwa ametumia mikono yake kufunika jicho lake la kushoto na akakimbizwa hospitalini.
"Kwa viganja vya mkono wangu, nilihisi mboni ya jicho ikiwa nje na kukaa upande mmoja wa uso," aliambia Radio Sport ya New Zealand.
"Bado jicho hilo lilikuwa linaona."
"Nakumbuka nikifikiria, bwana we ... hii ni hali mbaya, lakini nilihisi kwamba lilikuwa jambo la kushangaza na hapo ndipo niliingiwa na wasiwasi kiasi."
Mchezaji huyo wa miaka 24 anasema anakumbuka kusikia mashabiki na wachezaji wake wakiingiwa na wasiwasi.
Alidhani hangeweza kuona tena na kwamba uchezaji wake ulikuwa umefikia kikomo.
"Nilipoingizwa kwenye gari la kubeba wagonjwa walinipa dawa za kupunguza maumivu na matoneo kadha ya dawa yenye chumvi machoni na nikasakia mboni ya jicho ikirudi ndani, jambo ambalo pia lilikuwa la ajabu."
"Najihisi mwenye furaha sana kuweza kufunga na kufungua macho tena, ni jambo la kushangaza."
Baada ya kuruhusiwa kuondoka hospitalini Alhamisi, aliandika kwenye Twitter kwamba "najihisi vyema" na akatumia picha za vibonzo maarufu kama emoji za mboni za jicho.
Mchezaji huyo kutoka jimbo la North Carolina, Marekani anatarajiwa kupona kabisa na huenda akarejea uwanjani kucheza hivi karibuni.
Tweet saying

Tuesday, October 18, 2016

Ipate hii ya mwanafunzi aliyejifunza kulawiti toka kwa wazazi wake

Wananchi mbalimbali wa mkoani Kilimanjaro, wakiwamo wasomi na viongozi wa dini, wametaka uchunguzi wa watoto wadogo kudhalilishwa kingono ufanyike katika shule zote za msingi.Hoja yao imetokana na taarifa kuwa baadhi ya watoto wa kiume katika Shule ya Msingi Kaloleni wamelawitiwa na wa kike kufanya mapenzi na watu wazima.Hata hivyo, baada ya Gazeti la Mwananchi kufanya mahojiano na baadhi ya wanafunzi, mmoja alikiri kufanyiwa kitendo hicho na mwanafunzi mwenzake kwenye makalavati ya barabarani.Alipoulizwa alijifunzia wapi mchezo huo alisema, “nilikuwa nawaona baba na mama wanafanya ndiyo nikaamua nijaribu. Lakini toka tupelekwe polisi nimeacha kabisa huo mchezo.”Taarifa za shule hiyo ambazo zimethibitishwa na viongozi wa Serikali, zimekuja miezi minane tangu vitendo vya aina hiyo vibainike katika Shule ya Msingi Msaranga katika Manispaa ya Moshi.Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema suala hilo liligunduliwa na walimu wakati wakiwahoji wanafunzi ambao maendeleo yao kitaaluma yalionekana kushuka.


Ifuatilie vizuri habari hii katika Gazeti la Mwananchi...

WAFANYAKAZI NEW HABARI CORPORATION HATARINI KUWA VIZIWI

 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe John L. Kayombo (Kushoto) akiwa na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dkt Mariam Malliwadh mara baada ya kuwasili katika kampuni ya New Habari Corparation
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe John L. Kayombo akisikiliza kelele hizo ambazo zimekuwa zikiwasumbua wafanyakazi wa kampuni hiyo
Kelele ziosizo za kawaida huenda zikawasababishia wafanyakazi wa Kampuni ya New Habari Corparation matatizo ya kutesikia kutokana na kutokuwa na vifaa madhubuti vya kuzuia kelele hizo.
Hayo yamebainika wakati wa Ziara ya ghafla iliyofanywa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe John L. Kayombo ambapo miongoni mwa mambo yaliyobainika ni pamoja na kelele hizo zisizo za kawaida ambazo zinazotolewa na mtambo wa kutengeneza magazeti katika kampuni hiyo ambazo zinahatarisha uwezo wa wafanyakazi wa kusikia .
Ziara ya Mkurugenzi Kayombo ya kutembelea katika kampuni hiyo imekukuja muda mfupi baada ya kusikia vilio vya wananchi na wafanyabiashara wanaoishi jirani na kiwanda hicho.
Baadhi ya wananchi wanaofanya biashara jirani na eneo hilo wamesema kuwa kwa muda mrefu wametoa malalamiko yao lakini hayakufanyiwa kazi, hivyo kuamua kufikisha kwa kiongozi shupavu mwenye nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi Mh. John Kayombo.
Baada ya malalamiko ya wananchi kumfikia ,bila kupepesa macho Mkurugenzi Kayombo akaenda New Habari House bila kutoa taarifa kwa uongozi wa kiwanda kwa nia ya kuona hali halisi.
Akiwa kiwandani hapo Mkurugenzi Kayombo alikagua maeneo mbalimbali yanayozunguka kiwanda na hatimaye akafika kwenye mashine inayochapisha magazeti yanayotolewa na kampuni hiyo.
Mashine hiyo ilikuwa inapiga kelele hali ambayo sio rahisi kwa binadamu kukaa eneo hilo lakini alikuta wafanyakazi wakiwa hapo tena bila kifaa chochote cha kuzuia au kupunguza sauti hizo.
'' Hili jambo sio zuri haiwezekani mashine ipige kelele kiasi hiki huku wafanyakazi wakiendelea kuzalisha magazeti,huu ni ukatili na ni kwenda kinyume na haki za binadamu"alisema Kayombo.

Monday, August 1, 2016

Pitia hii ya mikojo ya walevi kutumika kutengenezea bia!


Inaweza kukushangaza kwa namna yake lakini unaambiwa watumiaji wa pombe sasa wataweza kupata auheni ya bei ya vinywaji, baada ya wanasayansi kugundua kifaa maalumu kitakachotumika kubadilisha mikojo ya walevi kutumika kutengenezea bia.

Kugunduliwa kwa kifaa hicho ni mkombozi kwa wamiliki wa viwanda vya pombe ambapo wataweza kupata malighafi ya kutengenezea bia kwa urais.

Kinatarajiwa kufungwa kwenye vyoo vya baa mbalimbali ili kurahisisha upatikanaji wa mikojo hiyo ya walevi.

Kifaa hicho ambacho kitakuwa kikitumia umeme wa jua pia kitakuwa na uwezo wa kubadili mikojo hiyo kutumika kama maji ya kunywa.

Timu ya watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Ghent nchini Ubeligiji, walisema kifaa hicho kitaanza kutumika hususan maeneo ya mijini kwenye nchi zinazoendelea.

Licha ya kuwepo kwa mashine maalum yenye uwezo wa kutibu maji machafu ikiwemo mkojo kisha kutumika kwa matumizi mengine muhimu ya binaadamu, wataalamu hao wamesema kifaa hicho walichokigundua kinauwezo zaidi wa kuyatibu maji hayo bila kutumia nguvu ya umeme.

Dk. Sebastiaan Derese, alisema kifaa hicho kitakuwa kikitunza mikojo kwenye tangi maalum ambalo litatumika kutibu kisha kutumika kama malighafi ya kutengenezea bia.

Kwa mara ya kwanza kifaa hicho kilianza kutumika kwenye tamasha la muziki ililofanyika mjini humo ambapo jumla ya lita 1000 za mikojo, zilikusanywa kisha kutengenezewa bia.

Alibainisha kuwa, bia zilizotengenezwa kupitia mikojo hiyo imewavutia wanywaji wengi hususan kwenye matamasha mbalimbali.

Monday, July 18, 2016

Jamaa kawashambulia abiria ndani ya Treni akiwa na kisu na shoka

Mtu mmoja aliyekuwa na Kisu na Shoka amewashambulia abiria waliokuwa kwenye Treni Kusini mwa Ujerumani usiku wa jumatatu na kuwajeruhi watu wanne kabla yeye kupigwa risasi na Polisi na kufa alipokuwa akikimbia baada ya tukio hilo.
Polisi wa mjini Wuerzburg wameeleza kwenye ukurasa wao wa Facebook kuwa abiria watatu wamejeruhiwa vibaya na wengine 14 wanapata msaada wa kitabibu kutokana mshtuko walioupata.
Polisi wamesema bado hakuna taarifa yeyote kuhusu sababu ya kutekelezwa kwa shambulio hilo.
vyombo vya habari vya Ujerumani vimemnukuu msemaji wa wizara ya mambo ya ndani mjini Bavaria kuwa mtu huyo ni mvulana wa miaka 17, mkimbizi mwenye asili ya Afghanistan.
Mwaka jana Ujerumani iliwaandikisha wahamiaji milioni moja waliokuwa wakiingia nchini humo, zaidi ya 150,000 raia wa Afghanistan.
Tangu mashambulizi ya hivi karibuni ya wanamgambo wa kiislamu nchini Ufaransa, kumekuwa na hali ya hofu ya kutokea mashambulizi kama hayo nchini Ujerumani, lakini mpaka sasa hakuna ishara zozote kuwa shambulio hilo lilikua la kigaidi.

Sunday, July 17, 2016

Sokwe aliyezaliwa mwaka 1975 afanya Birthday...!


Duniani kuna mambo ambayo yanatokea kila siku ya kufurahisha, kuhuzunisha, kuelemisha au kuburudisa,sasa unaambiwa Sokwe mmoja nchini Uingereza amesherehekea umri wa miaka 40 na amini usiamini Sokwe huyo alizaliwa mwaka wa 1975!
Salome, kama anavyojulikana sokwe huyo aliyezaliwa katika hifadhi ya Bristol Zoo Gardens ni mwerevu sana hasa ikiwa unampa chemsha bongo na kisha umpe chakula anachokipenda zaidi ,,,ndipo utajua uweledi wake.
Kama kutambua umri wake, wahudumu wa hifadhi hiyo walimuandalia dhifa kusherehekea kutimiza.
 
Kama sherehe zote za sikukuu ya kuzaliwa, Sokwe huyo alinunuliwa keki pipi ndizi na hata maua ya waridi.
Salome alikubali sokwe wenzake watano akiwemo mwanaye wa tatu Kukena mwenye umri wa miaka 4 kula keki hiyo.
Msimamizi wa hifadhi hiyo ya wanyama Lynsey Bugg, amemmiminia sifa kochokocho Salome.

Salome anawapenda sana wanawe na hata anamuheshimu sana babake watoto wake''
''ni jambo la kufurahisha sana kumuona Sokwe kama huyu akigonga miaka 40''.

Wednesday, July 6, 2016

Video Interview: Diamond na sanamu za mafuvu ofisini kwake


Ni kweli Freemasonry kama ilivyo maana yake kwanza ilkuwa ni kundi la mafundi waashi (masons) au wajenzi kuwa lugha nyingine. Walikuwa ni wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa mahekalu na mabenki ya zama hizo zinazoitwa kwa kizungu (medieval times).
Lakini miaka ya hiki karibuni kumekuwa na imani kwa watu kuwa freemasons ni imani ya kishetani ambayo imekuwa ikitumiwa na mastaa wakubwa duniani ili kufanikiwa zaidi kipesa na kuwa mashabiki wengi.
Hakuna aliyewai kuthitisha kwamba ni freemasons kama baadhi ya mitandao inavyoripoti, lakini wadau mbalimbali wa mambo duniani wamekuwa wakitoa na kuonyesha alama mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumiwa na watu hao ili kutambuana.
Diamond Platnumz Jumanne hii alipost video instagram akiwaeleza mashabiki wake kuhusu kuchelewa kwa kazi yake mpya ambayo ilikuwa itoke wiki iliyopita, lakini ndani ya video hiyo ambayo inaonyesha kuchukuliwa ofisini kwake, imeonyesha sanamu za mavufu mawili ya watu na kuibua maswahi mengi kwa mashabiki huwenda zikawa alama za kifremasons ambazo zimekuwa zikitumika na mastaa mbalimbali waliofanikiwa duniani.

Monday, July 4, 2016

Hii ni ya Mwanamke kuzalisha mayai ya bintiye aliyefariki...!


Mwanamke ambaye anataka kutumia mayai ya uzazi ya bintinye ili kumzaa mjukuu wake ameshinda kesi mahakamani na kuruhusiwa kufanya hivyo.
Mwanamke huyo wa umri wa miaka 60 alikuwa amekatazwa kupeleka mayai ya bintiye kwenye kliniki moja nchini Marekani hali iliyosababisha akate rufaa.
Bintiye ambaye aliaga dunia mwaka 2011, anaripotiwa kumuambia mamake amzalie watoto wake. Lakini mamake alishindwa katika kesi mwaka uliopita.
Hata hiyo aliruhusiwa kupinga hukumu hiyo katika mahakama ya rufaa mjini London mbele ya jopo la majaji watatu.
Mwaka 2014 halmashauri inayohusika na mayai ya uzazi, ilisema kuwa mayai hayo hayangetolewa mjini London, kwa sababu bintiye hakuwa ametoa idhini kamili kabla ya kifo chake akiwa na umri wa miaka 28.
Lakini kwenye kesi ya sasa mawakili waliawaambia majaji kuwa, mwanamke huyo alikuwa anataka kutimiza matakwa ya bintiye ya kuzaa mtoto akitumia mayai yake na kisha amlee mtoto huyo.

Saturday, April 16, 2016

Hapa ni Picha za miongoni mwa vyoo bora zaidi duniani...!!!!

Vyoo

Kuna mambo mengi yaliyopo kwenye ulimwengu ambayo kuna watu wanayatizama sana kwa maana zao, sasa mwongozo wa vyoo 100 bora zaidi duniani uliochapishwa na kampuni ya usafiri ya Lonely Planet umeorodhesha vyoo vya kila aina ambavyo bila shaka vina uwezo wa kuwaacha wasafiri vinywa wazi au kuwa na kumbukumbu za kusalia nazo daima.
“Vyoo ni dirisha la kuingia ndani katika moyo wa pahala Fulani. Isitoshe, bila kujali unavipa jina gani, vyoo huwaweka watu wote katika ngazi sawa,” kitabu hicho kinasema.
Hapa chini ni baadhi ya vyoo vilivyo kwenye mwongozo huo.
VyooImage copyright
Vyoo hivi vinapatikana Chott, Tunisia katika ziwa la maji ya chumvi lililokauka. Hapa ndipo video ya nyumba ya Luke Skywalker katika filamu ya Star Wars ilichukuliwa.
VyooImage copyright
Vyoo hivi katika eneo la Bahia, Brazil vimo katika kituo cha kutunza kasa.
Image copyrigh
Choo hiki ambacho kinapatikana eneo lenye mandhari ya kupendeza kinapatikana Uswizi. Hapa ni mita 2,7000 katika milima ya Alps.
Image copyrig
Choo hiki katika duka la Standard Grill katika mtaa maarufu wa kufungia nyama New York kimeelezwa na wengi kama choo kinachokanganya ubongo.
Image copyrigh
Vyoo hivi vijulikanavyo kama Between The Waters vinapatikana Emscherkunst nchini Ujerumani.
Image copyrigh
Hapa ni Wellington, New Zealand. Kwa kutazama picha, ni vigumu kuelewa vyoo hivi hutumiwa vipi. Lakini waliozijenga walitaka zifanane na miguu ya kambakoche.