Latest News

Tuesday, June 6, 2017

Nabii Wa Ajabu Aonekana Kwa TB Joshua!


Nabii alisababisha utata nchini Afrika Kusini, mwaka 2015, baada ya kuwafanya waumini wake kula nyoka, panya na nywele ameonekana kwenye ibada nchini Nigeria ya muhubiri maalufu TB Joshua.

Muhubiri Penuel Mnguni ameoneaka katika ibada iliyoongozwa na mhubiri TB Joshua katika kanisa lake na aliweza kutoa ushuhuda umaosema kuwa ”nilianza kutizama TV za Emmanuel TV na kumsikiliza nabii TB Joshua, nikafahamu kuwa nilichokuwa nikifanya haikiendani na maandiko. Na nilivyofahamu kuwa lilikuwa shambulio nikaja hadi kwa TB Joshua ili anikomboe.”

Kupitia akaunti yake ya twitter Muhubiri Joshua aliweza kutwit kwa kuonesha kuwa alimpokea mchungaji huyo katika kanisa lake.
Nabii Mngui amebadilisha moyo wake, kwa mujibu wa gazeti la Citizen baada ya kujikuta akiandamwa mara kwa mara na kupelekea kushtakiwa na chama cha kupambana na dhuluma dhini ya wanyama (Society for the Prevention of Cruelty to Animals) Afrika Kusini, hata hivyo mastaka hayo yalifutwa mwaka 2015 Julai baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha.

No comments:

Post a Comment