Serikali imesisitiza kwamba, katazo la Unywaji, Usambazaji na Uzalishaji wa Pombe aina ya ‘Viroba’ uko palepale na utekelezaji wake utafanyiwa unaanza Machi 1.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa rais (Mazingira na Muungano) Januari Makamba, amesema kuwa utekelezaji wa maamuzi ya Serikali kuhusu usitishaji uingizaji, uzalishaji, uuzaji na matumizi ya vifungashio vya plastiki vya kufungia pombe kali ‘viroba’utaanza rasmi tarehe 01 Machi, 2017, katika Mikoa yote ya Tanzania Bara.
Tizama hapa Mh January Makamba akiongelea suala hilo mbele ya waandishi wa habari:-

No comments:
Post a Comment