Latest News

Wednesday, July 13, 2016

Usipitwe na chanzo cha kifo cha Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki


Ninazo taarifa za kifo cha Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Burundi Hafsa Mossi kuuawa na watu wasiojulikana mjini Bujumbura, Mossi, aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki katika serikali ya nchi hiyo, aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya Gihosha, eneo la Nyankoni.
Gari la marehemu Mossi lililokutwa baada ya tukio
Mbunge huyo aliwahi pia kufanya kazi na idhaa ya Kiswahili ya BBC, Msemaji wa rais wa Burundi Willy Nyamitwe kupitia account yake ya Twitter amesema amesikitishwa sana na mauaji ya mwanasiasa huyo.

No comments:

Post a Comment