Latest News

Tuesday, April 19, 2016

Azam imeshakwama michuano ya CAF, Idadi ya magoli iliyofungwa ninayo hapa!

Kwa namna moja au nyingine nchi yetu ilifanikiwa kuwa na wawakilishi kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika Azam FC, lakini timu hii imetupwa nje ya michuano ya hiyo baada ya kuchapwa kwa magoli 3-0 na
Esperance ya Tunisia kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa Tunis, Tunisia.
Azam walikomaa kipindi cha kwanza na kufanikiwa kwenda mapumziko wakiwa hawajaruhusu goli hata moja licha ya mashambulizi makali ya mara kwa mara kufanywa kwenye goli lao lakini golikipa Aishi Manula alikuwa imara kuondosha hatari zote na kuiweka Azam salama.
Dakika ya 49 kipindi cha pili Esperance walipata bao la kuongoza lililopachikwa kambani na Saad Bguir kisha Jouini akaiandika bao la pili na Ben Yousef akaihakikishia timu yake kusonga mbele baada ya kufunga bao la ushindi dakika tisa kabla ya mchezo kumalizika.
Benchi la ufundi la Azam chini ya Stewart Hall lilifanya mabadiliko kujaribu kubadili matokeo kwa kuwapumzisha Farid Musa, Salum Abubakar ‘Sure Boy’na Wazir Salum huku nafasi zao zikichukuliwa na Hamisi Mcha, Himid Mao na Didier Kavumbagu lakini bado mabadiliko hayo hayakumlipa kocha huyo raia wa England.
Esperance imeitupa Azam nje ya mashindano kwa jumla ya magoli 4-2 baada ya kucheza mechi mbili. Mchezo wa kwanza Azam ikiwa nyumbani ilishinda kwa magoli 2-1 lakini leo imejikuta ikikubali kuchapwa magoli 3-0 ndani ya dakika 32 na kuyaaga mashindano rasmi.

No comments:

Post a Comment