Latest News

Wednesday, April 20, 2016

Faraja imerudi tena kwa Barca baada ya kujirudishia kwa Deportivo {VIDEO}


Klabu ya Barcelona ilipata kichapo kutoka kwenye klabu ya ValenciaAtletico MadridReal Sociedad na kuondolewa katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya na klabu ya Atletico Madridsafari hii Barca wamerudi tena dimbani
kucheza dhidi ya klabu ya Deportivo la Coruna.
Katika mchezo huo wa 34 kwa FC Barcelona wameonesha hasira na kuifunga Deportivojumla ya goli 8-0, ushindi ambao umekuja siku chache baada ya kufungwa na klabu yaValencia goli 2-1. FC Barcelona wameifunga Deportivo na kufikisha jumla ya point 79.
Magoli ya FC Barcelona yalianza kufungwa dakika ya 11 na 24 kupitia kwa Luis Suarezambaye alifunga tena magoli mengine mawili dakika ya 53 na 64 baada ya Ivan Raktickupachika goli la tatu dakika ya 47, Lionel Messi goli sita dakika ya 73 na Neymarakahitimisha kwa kufunga magoli mawili ya mwisho dakika ya 79 na 81.

Tizama video ya magoli hapa chini:-

No comments:

Post a Comment