Latest News

Monday, April 18, 2016

IKUFIKIE HII YA HARMONIZE KUWEPO KWENYE PROJECT MPYA YA DULLY SYKES

Tunaona wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya wenye majina wamekuwa wakiwatafuta wasanii wenzao wenye majina pia pale wanapokua wanataka kuachia ngoma ya
kushirikisha. Harmonize nimsanii mwenye jina kwa sasa lakini si kama wasanii wakongwe ukizingatia umaarufu wake umekuja hivi karibuni, Lakini msanii Dully Sykes anataka kufanya naye kazi.

Hii ni project mpya ya Dully ambayo kupitia East africa radio anasema kuwa ameamua kumchukua Harmonize kwakuwa kuna vitu vingi amefanya na Diamond platnumz na kusababisha kuambulia matunda yake hivyo akaona siyo mbaya kumrudishia fadhila kwa kumchikua kijana wake na kufanya naye kazi.

Unadhani project itakua poa na kutrend kwa muda mrefu?, acha maoni yako!

No comments:

Post a Comment