Latest News

Friday, May 27, 2016

Kuhusu video ya wimbo wa Pamoja, Marlaw kasema haya!


Marlima Rawrence ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutokea mkoani Iringa, ameizungumzia idea ya wimbo wake mpya ‘Pamoja’ aliyomshirikisha mtayarishaji mkongwe wa muziki Fundi Samweli pamoja na maandalizi ya video yake.
Kupitia instagram, Marlaw ameandika ujumbe huu ili kufafanua maana ya wimbo huo:
Nilimwambia Fundi Samweli kwamba nina wimbo unaitwa ‘Pamoja’ na itabidi tuuimbe pamoja ili kuumaanisha. Yeye awe upande wa kutetea UPWEKE na mimi upande wa kutetea PAMOJA. Imewezekana na imetokea kuwa wimbo poa sana pale Jahman Records tukiwa na ushirikiano mzuri kutoka kwa Big Jahman. Wazo la wimbo PAMOJA ni kwamba mara nyingi watu wakiwa kwenye hasira ni rahisi sana kusema “bora pekeangu” au vinginevyo ambapo ni kauli inayopelekea kufikiria na kuamini kwamba inawezekana mtu mmoja kuwepo bila uwepo wa mtu mwingine. Sasa ukweli ni kwamba wote tunategemeana. Uwepo wa mtu mmoja ni muhimu kwa mwingine. Kwenye albamu yangu ya “Bembeleza” kuna wimbo unaitwa “Maisha” mule niliuliza ‘Itakuaje ukiamka asubuhi ukute dunia nzima watu hawapo umebaki mwenyewe? Utawezaje kufa ujizike mwenyewe?’ Haiwezekani kwasababu tunategemeana. Huwezi kuja duniani mwenyewe bila kuzaliwa na mtu mwingine ambaye ni mama, nae atakwambia kuna baba ambapo na wao pia wamezaliwa basi inaendelea hivyo na kadhalika… Hivyo basi haukamiliki mwenyewe. Pamoja ipo baina yetu.
Video ya wimbo Pamoja ambayo inatoka kesho, imeongozwa na director Kris Erah.

No comments:

Post a Comment