Baada ya msanii Nay wa mitego kufungiwa nyimbo zake mbili sasa taarifa kutoka Baraza la sanaa Tanzania, BASATA zinasema kuwa msanii huyo hatakiwi kujihusisha na kazi ya muziki.
Chanzo kimoja cha habari Jijini Dar es Salaam kimehojiana na BASATA na taarifa ni hii hapa chini:-
‘Ni kweli kwamba tumetoa tamko hilo tulifuata sheria na kanuni labda nizungumzie kile ambacho kilichotufanya tuchukue maamuzi hayo, moja nadhani mnakumbuka ilikuwa tarehe 16 mwezi wa saba Baraza la Sanaa ilitoa taarifa kwa umma kuhusu kuufungia wimbo wa Msanii huyo Pale Kati kutokana na maudhui ya mule ndani’-Godfrey Mngereza
‘Kwahiyo hivi karibuni tulikaa tena kikao na akakiri kwamba kweli wimbo wake haupo kimaadili pia tukaona ngoja tumfungie kwa muda usiojulikana kutokana na tamko la wizara kuhusu maadili ya wimbo huo, alitoa wimbo wa Pale Kati na kuusambaza bila Baraza la Sanaa kuwa na taarifa yoyote kwahiyo ndio maana tukaona ngoja tumpe adhabu’- Godfrey Mngereza
No comments:
Post a Comment