Akitokea benchi zikiwa zimesalia dakika 10 mechi kumalizika, Mbwana Samatta amefunga bao lililoipa ushindi Genk kwenye mchezo wao wa kwanza wa ligi ya Ubelgiji (Belgium Pro League) na kuisaidia timu yake kupata ushindi wa magoli 2-1 wakati timu yake ikicheza dhidi ya KV Oostende.
Nikolaos Karelis alianza kufunga bao la kwanza dakika ya 50 kipindi cha pili kisha Mbwana Samatta akapachika bao la pili dakika ya 90+1.
Oostende walipata bao la kufutia machozi dakika ya 90+3 lililofungwa na Mzimbabwe Knowledge Musona na mpaka mwamuzi wa mechi hiyo anamaliza pambano hilo matokeo yakabaki Genk 2-1 Oostende.
Genk wamefanikiwa kupata pointi tatu na kukaa nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi moja kwenye ligi hiyo ambayo ilianza msimu mpya jana Jumamosi. Timu ambazo zipo nafasi ya juu ya Genk zinatofautiana kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga lakini pia herufi za kwanza za majina zimetumika kupanga ni timu gani ikae juu ya nyingine.
No comments:
Post a Comment