Jana
ziliripotiwa habari za kutekwa kwa madereva wa malori kutoka Tanzania na
Kenya kutekwa na kundi la waasi nchini Congo. Leo September 16 habari
zilizoripotiwa na BBC Swahili zimedai kuwa watu wameokolewa na jeshi la
nchi hiyo.
BBC
imezungumza na waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo ambapo kuwa
madereva wote wameokolewa na vikosi vya jeshi la nchi hiyo na wako
salama. BBC imesema utekaji wa madereva hao ulifanywa na watu wenye
silaha katika kijiji cha Matete kuelekea Namoya kilichopo Mji wa Kivu
Kusini Mkoa wa Manyema.
Waziri wa
Mambo ya Ndani wa Congo alipoongea na BBC kwa njia ya Simu, amesema ni
magari saba ya kampuni ya Simba inayomilikiwa na mfanyabiashara Azim
Dewji kutoka Tanzania ndio yaliyochomwa.
Waziri huyo amesema tukio hilo halijafanywa na waasi kama ilivyoanza kuripotiwa, ila ni majambazi tu ndio waliofanya tukio hilo.
'Ni
majambazi tu wanatoka porini walipoona magari yanatembea
wakayasimamisha katikati ya pori na kuangalia kama kuna pesa
wanyang’anye lakini hawakukuta pesa wakaamua kuwachukua madereva na
kukimbia nao porini kisha wakayachoma magari 6 na moja halikuteketea'.
Waziri Mambo ya Ndani Congo amezungumza hayo.
No comments:
Post a Comment