Latest News

Friday, September 16, 2016

Video: Anyofolewa ulimi kwa kunyonyana ndimi na mwanamke


Hii ni habari iliyoripotiwa na kituo cha TBC, ambapo kijana Said Mamba (24) mkazi wa Mandewa, Manispaa ya Singida, amelazwa hospitali baada ya kung’atwa sehemu ya ulimi wake na mwanamke waliyekuwa wakinyonyana ndimi.
Mamba ambaye kwa sasa hawezi kuzungumza, aling’atwa Septemba 12, saa 3:30 usiku wa kumkia Sikukuu ya Idd el Hajj.

Alisema siku ya tukio alikutana na mwanamke huyo kwenye grosari iliyopo eneo la Mandewa na baadaye mwanamama huyo alimwomba amsindikize nyumbani kwake.


“Nilikubali kumsindikiza, tukiwa njiani aliniomba tufanye mapenzi. Nilipokataa alinilazimisha na baada ya kuona sitaki aliomba tuagane kwa kunyonyana ndimi, nilikubali ombi hilo,” alisema.

Mamba alisema wakati wakiendelea, mwanamke huyo alianza kumvua mkanda wa suruali lakini alimzuia ndipo alipomng’ata ulimi na kuondoka na kipande.

No comments:

Post a Comment