Siku ya jana October 8, 2016 chama cha ACT Wazalendo kilifanya mkutano mkuu wa kidemokrasia ambapo umewakusanya wanachama na wageni mbalimbali kutoka nchi na vyama marafiki kwa ajili ya kubadilisha uzoefu katika nyanja mbalimbali, Sasa mmoja wa walioalikwa katika mkutano huo ni mwenyekiti wa chama cha Labour Kenya, Ababu Namwamba, mbele ya waaandishi wa habari Namwamba ameulizwa jinsi Wakenya wanavyochukulia utendaji wa Rais Magufuli.
Namwamba anaeleza kuwa Wakenya wanaheshimu uamuzi wa kidemokrasia, hususan kwa watanzania kuamua viongozi wao. Kwahiyo walipoamua kuwa rais Magufuli ndiye kiongozi walifanya uchaguzi sahihi.
" Basi wakenya waliheshimu uamuzi wa watanzania na wamemtambua rais Magufuli kama rais wa Tanzania aliyechaguliwa kidemokrasia." Alisema Namwamba.
Bonyeza play kusikiliza...............
No comments:
Post a Comment