Latest News

Monday, October 10, 2016

Katika kukomesha suala la dawa za kulevya, mbinu mpya zimegunduliwa na jeshi la polisi!

Tume ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini imeanza kutumia mbinu mpya kudhibiti dawa hizo katika mipaka iliyopo hapa nchini ikiwemo mipaka ya Tunduma na Kasumulu katika mikoa ya Mbeya na Songwe.
Mkuu wa kitengo cha kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya hapa nchini, Kamishna msaidizi wa jeshi la polisi Mihayo Misikela amesema mbinu hizo zimeanza kutolewa kwa wakuu wapelelezi wa jeshi la Polisi ngazi ya wilaya na mikoa ili kuwabaini wasafirishaji na waingizaji wa dawa za kulevya hapa nchini.
Wakati huohuo mwakilishi wa mkemia mkuu wa Serikali Bwana Aloyce Ngonyani amesema kuwa wametoa vifaa mbali mbali vya utambuzi wa awali wa dawa za kulevya kwaajili ya makundi ya dawa mbali mbali na utambuzi wa kemikali
Mipaka ya Kasumulu na Tunduma ndio mipaka maarufu inayosemekana inapitisha zaidi madawa ya kulevya.

No comments:

Post a Comment