Kama umekuwa karibu na mitandao mbali mbali basi lazima utakua hukupitwa na ile habari ya kijana kutobolewa macho huko Buguruni Dar Es Salaam. Sasa hapa ni taarifa za majibu ya madaktari juu ya uchunguzi wa Macho ya kijana Said maaarufu kama Baba D ambaye alipata mkasa wa kushambuliwa na mtu anayefahamika kwa jina la Scorpion, kisha kutobolewa macho yote mawili hali iliyopelekea kutoona.
Jitihada zilizofanywa na Serikali ya mkoa wa Dar es salaam zikiongozwa na mkuu wa mkoa Paul Makonda ili kuweza kumsaidia kijana huyo zilifanikiwa kumfikisha katika Hospitali ya Muhimbili ambako alifanyiwa uchunguzi wa kina ili kujua kama kuna uwezekano wowote wa kumrejeshea uwezo wa kuona.
Hii ni video ya maelezo yote.....( Globalpublisherstz ).
No comments:
Post a Comment