Kampuni ya udalali ikishirikiana na NHC ilitoa vifaa hivyo nje huku Wafanyakazi wa ofisi hiyo wakiwa kwenye hali ya kushangazwa ambapo meneja wa kitengo cha kukusanya madeni NHC alisema taratibu zote zilifuatwa na Mbowe Hotels walishapewa notice sababu Mbowe anadaiwa.
Mbowe alifungua kesi mahakama kuu kitengo cha ardhi kupitia kampuni yake ya Mbowe Hotels Ltd akipinga uamuzi wa NHC kumuondoa katika jengo, leo October 18 2016 mahakama hiyo imefutilia mbali maombi hayo.
Katika uamuzi huo uliotolewa na mahakama hiyo na Jaji Sivangila Mwengesi amesema kuwa maombi yake hayana msingi na hivyo jaji Mwangesi amekubaliana na hoja za NHC na kusema kuwa aliondolewa katika jengo kisheria.
No comments:
Post a Comment