Upande mashitaka uliiomba mahakama kuliondoa shitaka la unyanganyi wa kutumia silaha linalomkabili Salumu Njwete kwa nia ya kutotaka kuendelea nalo.
Kutokana na ombi hilo hakimu Adelf Sachole alikubaliana na ombi hilo kuliondoa shitaka hilo kupitia kifungu cha 91 (1) ambapo kinampa mamlaka mkurugenzi wa mashitaka (DPP) kuondoa mashitaka muda wowote ilimradi isifike kwenye hukumu.
Baada ya saa kadhaa alifunguliwa shitaka hilohilo tena kwa hakimu mwingine Frola Haule, shtaka hilo ni la unyang’anyi kwa kutumia silaha alilolifanya September 6 2016 Buguruni sheli Dar es salaam na kuchukua vitu vyenye tahamani ya sh 476,000, Salumu alikana mashitaka hayo.
Kutokana na kesi inayomkabili kisheria haina dhamana amerudishwa rumande na kesi hiyo itatajwa tena November 2 2016
No comments:
Post a Comment