Leo mchana Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Freeman Mbowe alifika kwenye kituo cha Polisi kati Dar es salaam kutii wito wa kuhojiwa na Polisi kwenye sakata la dawa za kulevya baada ya jina lake kutajwa kwenye orodha February 8.
Baada ya kukaa kituoni hapo kwa zaidi ya dakika 60, Waandishi wa habari waliokua nje ya eneo hilo walishuhudia Mwenyekiti huyo akichukuliwa na Gari aina ya Land Cruiser iliyofatwa na magari mengine nyuma yake na kuelekea ambako Waandishi hawakufahamu mara moja.
Utaratibu huu wa kuwaondoa kituo cha Polisi kati ulifanyika pia kwa Askofu Gwajima na Mfanyabiashara Yusuph Manji ambapo baadae ilikuja kujulikana walipelekwa kwa Mkemia mkuu kupimwa kama wanahusika na utumiaji wa dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment