Latest News

Tuesday, February 21, 2017

Ripoti baada ya Freeman Mbowe kutoka mahakamani leo


Mahakama kuu Dar es salaam imetoa zuio la muda kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kutokamatwa na Polisi au kuwekwa kizuizini mpaka mpaka maombi yake yataposikilizwa Ijumaa ya Feb 24 2017.

Mbowe alikamatwa jana Jumatatu jioni wakati akienda kujisalimisha polisi na kupekuliwa nyumbani kwake kabla ya kuhojiwa hadi alipoachiwa usiku wa manane.
Ofisa habari wa chama hicho, Tumaini Makene amethibitisha  taarifa za kuachiwa mwanasiasa huyo kuwa ni za kweli.
Hata hivyo, taarifa iliyosambazwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu kupitia mitandao ya kijamii imesema kuwa chama hicho kitatoa taarifa zaidi juu ya tukio hilo leo.
“Tunawashukuru wote kwa sala, maombi na subira na hivyo kuhitimisha salama saa kumi za mwenyekiti wetu kuwa chini ya Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam,” Mwalimu amesema.

No comments:

Post a Comment