Latest News

Monday, February 20, 2017

Shamsa Ford ameandika haya baada ya mumewe kuhusishwa na ishu ya madawa ya kulevya


Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford ameonyesha kusikitishwa na ishu iliyomkuta mumewe kwa ishu nzima ya madawa ya kulevya na ameandika maneno haya kwaajili yake


Nilipoolewa nilijua ipo siku nitapitia hivi vitu huzuni,furaha, maudhi, kudharauliwa, kuchekwa na nk.ila pamoja na yote hayo haitabadilisha mapenzi yangu kwa mume wangu kipenzi. Nina amini kuwa wewe ni mume aliyenipa Mungu na wala Mungu hakutukutanisha kwa bahati mbaya.

Dunia nzima ikuzomee na kuamini kile wanachoamini lakini jua una mke anayekupenda kwa dhati .Ninakujua, ninakuamini na kukupenda sana ndomaana niliolewa na wewe kwasababu nilijua utakuwa baba bora kwa mwanangu kama ambavyo ulivyo sasa..

Nina amini Mungu anapotaka kukupeleka sehemu anayoitaka yeye lazima akupitishe kwenye mitihani. Hii ni mitihani ya Mwenyezi Mungu na nina imani in shall ah yatapita..Nakupenda sana mume Wangu kipenzi Rashidi..

No comments:

Post a Comment