Latest News

Monday, February 20, 2017

VPL: Azam bado baba lao kwa Yanga na Simba


VPL
Ligi Kuu Vodacom
Matokeo:
Jumapili Februari 19
Ndanda FC 0 African Lyon 0
Mtibwa Sugar 0 JKT Ruvu 0
Azam FC 2 Mwadui FC 0

AZAM FC Juzi Usiku wakiwa kwao huko Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam waliichapa Mwadui FC 2-0 na kujichimbia Nafasi ya 3 ya VPL, Ligi Kuu Vidacom.
Sasa Azam FC wamecheza Mechi 23 na wana Pointi 41 wakiwa nyuma ya Timu ya Pili Yanga waliocheza Mechi 21 na wana Pointi 50 huku Simba wakiwa kikeleni kwa kuwa na Pointi 51 kwa Mechi 22.
Katika Mechi ya Jana, Timu zote zilivaa Vitambaa Vyeusi mkononi na pia Vikosi vyote Viwili pamoja na Mashabiki wote Uwanjani walisimama kimya kwa Dakika 1 kwa heshima ili kuomboleza kifo cha Kiungo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Tukuyu Stars, Tanzania Prisons na Yanga, Geoffrey Boniface Mwandanji, aliyefariki dunia katikati ya Wiki hii. 
Azam FC walikuwa 1-0 mbele wakati wa Haftaimu kwa Bao la Dakika ya 24 la Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
Bao la Pili la Azam FC ni la kujifunga mwenyewe Mchezaji wa Mwadui FC Iddi Moby katika Dakika ya 88.
VIKOSI:
AZAM FC: Aishi Manula, Shomary Kapombe, Bruce Kangwa, Abbrey Morris, Yakubu Mohammed, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Samuel Afful, 62), Frank Domayo, Yahya Mohammed (Erato Nyon, 88), Ramadhani Singano ‘Messi’, Joseph Mahundi (Masoud Abdallah, 70).
MWADUI FC: Shaaban Kado, Nassor Masoud ‘Chollo’, David Luhende, Iddi Mobby, Malika Ndeule, Razack Khalfan, Abdallah Seseme, Awadh Juma, Paul Nonga (Salum Iyee, 18), Miraj Athuman na Hassan Kabunda
VPL.

Ratiba
Jumatatu Februari 20
Toto Africans v Kagera Sugar
Jumanne Februari 21
Mbao FC v Maji Maji FC
Jumamosi Februari 25
Simba v Yanga

No comments:

Post a Comment