Mkuu wa mkoa wa Dar-es-Salaam Paul Makonda amewataka wakazi wa jiji la Dar-es-salaam kulinda vyanzo vya maji kwani ukosefu wa maji unachangiwa na kuharibu vyanzo hivyo..Makonda ameyasema hayo leo katika wiki ya maji na kuongeza kuwa kuna baadhi ya sehemu watu wamekuwa wakiharibu miundombinu ya maji bila kutoa taarifa kwa mamlaka husika jambo linalopelekea uhaba wa maji katika maeneo hayo.
Amesema kuwa kwa sasa jiji la Dar-es-salaam lina uhitaji wa lita milioni 510 kwa siku ambapo lita 390 tu ndizo zinazozalishwa kwa sasa hivyo serikali imejipanga kipitia miradi yake mbalimbali kufikia mwaka 2020 tatizo la maji katika mkoa liwe limepungua kwa 95%.
Wiki ya maji duniani huazimishwa kila tarehe 16-22 mwezi march ya kila mwaka ambapo mwaka huu kauli mbiu yake ni"majisafi na majitaka-punguza uchafuzi yatumike kwa ufanisi.
Bonyeza Play hapa chini....
No comments:
Post a Comment