Serikali mkoani imepongeza jitihada za shirika la kimataifa la Heifer International kwa kuanzisha Mradi rafiki kwa vijana Mardi waushirikishwaji wa vijana Afrika Mashariki katika sekta ya Kilimo na mifuko (EAYIP).
Huku akitaka katibu tawala wa mkoa wa Iringa kuwawajibisha maofisa vijana wa Kilolo na Mafinga mji kwa kushindwa kuwapa vijana kipaumbele cha kushiriki uzinduzi huo.
Akizindua Mradi huo leo katika ukimbi wa siasa ni kilimo mjini Iringa, mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa mradi huo umekuja wakati ambao vijana wengi wanahitaji kuwezeshwa katika sekta ya kilimo na mifugo.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi mzuri wa Rais Dkt John Magufuli umedhamilia kuifanya Tanzania ya viwanda na jitihada hizo zimeanza kuonekana na kuwa mradi huo utawezesha vijana kunufaika na viwanda hivyo.
Hivyo alisema njia pekee kwa vijana kupiga hatua ni kujikita katika vikundi vya kiuchumi kwa kuanzisha kilimo na ufugaji na kwa kupitia mradi huo wa EAYIP vijana wawe na uhakika wa kupiga hatua.
“Nimefurahi sana kusikia ya kwamba shirika la Heifer International limeanzisha mradi huu wa miaka mitano wa ushirikishwaji wa vijana katika kilimo na mifugo lengo likiwa ni kuwezesha vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24 wapatao 10,453 nchini “
Alisema kuwa kundi la vijana waliolengwa na mradi huo linakabiliwa na changamoto nyingi sana lakini pia kundi hilo huwa linaachwa nyuma katika mambo mengi sana kwani mara nyingi hujitoa kama hawana uwezo wa kushundania fursa zinazojitokeza.
Masenza alisema kuwa serikali inatarajia kuona mradi huo unawasaidia vijana walengwa na kuwa wale wote watakaokwamisha mradi huo watawajibishwa.
Aidha alisema katika mkoa wa Iringa wapo wawekezaji katika sekta ya kilimo na mifugo hususani mazao ya mifugo kama vile maziwa kupitia kampuni ya Asas na kwa upande wa kilimo wapo kiwanda cha kusindika nyanya cha Dabaga hivyo viwanda hivyo ni fursa kwa vijana.
Japo alisema viwanda vyote hivyo vinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa mali ghafi na hivyo kupitia mradi huo vijana hawana budi kuongeza jitihada kubwa.
Kaimu meneja mkuu wa mradi huo Damas Damian alisema mradi huo utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa vijana na upo mikoa minne ambayo ni Iringa, Songwe, Njombe na Mbeya.
Kuwa kwa upande wa mkoa wa Iringa mradi huo uasimamiwa na shirika lisilo la kiserikali linalojihudisha na maendeleo ya vijana la Restless Development .
Kuwa kuna kuna fedha za kutosha kwa ajili ya kuwezesha mradi huo hivyo vijana.
Na Matukiodaima Blog
No comments:
Post a Comment