Wasanii watatu ambao ni Roma, Monii Central Zone, Bin Laden pamoja na
Imma ambaye ni mfanyakazi wa Mama mzazi wa mmiliki wa studio za Tongwe
Records J Murder, mpaka muda huu hawajaweza kupatikana na haifahamiki
wapi walipo baada ya kuvamiwa studio na kuchukuliwa na watu
wasiojulikana.
Mapema leo Mmiliki hiyo wa Tongwe Records alifika kituo cha Polisi
Osterbay na akanukuliwa akisema “Jana usiku baada
ya kutokea tukio nilienda kutoa ripoti pale polisi Osterbay kwahiyo leo
nilichoenda pale ni kujua mpelelezi wa kesi yangu ni nani nimpe
maelekezo wa vitu gani vime-happen pale studio.”
Sasa hapa pia Global Tv Online wamemtafuta mke wa Roma, naye ameweza kuzungumza yake ya moyoni kuhusu ishu hii.
Sikiliza hapa chini.
No comments:
Post a Comment