Kufuatia agizo la serikali lililotolewa na mkuu wa mkoa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu,juu ya wafugaji kuondoa mifugo yao katika mapori ya akiba na misitu ya hifadhi mkoani humo imepelekea operation ya kuwaondoa kwa nguvu kuanza kutekelezwa.
Kaimu mkurugenzi huduma za ulinzi wa wanyamapori Tanzania{TAWA}Faustine Masalu amesema kuwa march 30 mwaka huu operation hiyo ilianza rasmi ambayo itadumu kwa siku kumi na nne,na kufikia leo jumla ya mifugo 1,922 imekamatwa na watuhumiwa 19,watanzania 14,warundi 3 na wanyarwanda wawili na watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani siku ya kesho.
No comments:
Post a Comment