Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na askari katika jaribio la kupora fedha.
Watu
walioshuhudia tukio hilo lililotokea leo (Jumapili) wamesema mtu huyo
akiwa na wenzake walijaribu kupora fedha kwenye gari kabla ya kuwekwa
kwenye mashine ya kielektroniki ya kutolea fedha (ATM) ya benki moja
iliyopo katika jengo la makao makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini
jijini hapa.
Shuhuda wa tukio hilo, Leonard Macha amesema saa tatu asubuhi alisikia milio ya risasi eneo la jengo la Uhamiaji.
Macha
ambaye ni mlinzi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
lililo jirani na jengo hilo amesema polisi waliimarisha ulinzi eneo.
“Aliyekufa
aliamriwa asipite barabara hii, alipokataa kusimama polisi walipiga
risasi hewani, naye alipotaka kutoa bastola ndipo polisi walipomfyatulia
risasi na alikufa papo hapo,” anasema Macha.
Amesema wengine waliokuwa na mtu huyo walikimbia na mmoja amekamatwa.
Kamishna
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema
atazungumzia tukio hilo kesho atakapokutana na waandishi wa habari
ofisini kwake.
Source: Mwanachi
Source: Mwanachi
No comments:
Post a Comment