Latest News

Sunday, May 21, 2017

AUDIO: Waziri Nchemba Kazungumza Tena Kuhusu Mauaji Kibiti Na Mapambano Yanayoendelea


Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amesisitiza kushughulikia suala la mauaji yanayoendelea kutokea katika eneo la Kibiti Mkoani Pwani.

Akizungumza katika jiji cha Bungu, Kibiti  ilipo kambi ya Polisi wanaotunza amani, Waziri Nchemba amewataka polisi hao kusonga mbele katika mapambano ya  kuwasaka wauaji.
Aidha Nchemba amesema watu wanatakiwa kujiuliza kwanini wanaouawa ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na mtu ukiwa kwenye chama kingine unakuwa salama.
Amehusianisha pia mauaji haya na suala la ukataji mkaa, udini na uvyama ingawa akasema haiingii akilini mahusiano ya vifo na shughuli hizi.

Aidha Waziri Nchemba ameiagiza kamati ya ulinzi na usalama Kibiti kuweza kushughulikia mchezo huu ambao amesema kuwa ni wa muda tu, uweze kumalizwa mara moja.
"Lazima tuwapate hawa wanaofanya upuuzi wa aina hiyo". Alisema Mwigulu.

Sikiliza Hapa chini aliyoyazungumza.

No comments:

Post a Comment