Mashindano makubwa ya Afrika ya kuhifadhi na kusoma Quran Tukufu yaliyokuwa yakifanyika Uwanja wa Taifa tangu asubuhi, yamemalizika kwa washiriki kumaliza kusoma, ikisubiriwa majaji kumtangaza mshindi.
Mashindano hayo yamehudhuriwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Mufti Mkuu Aboubakar Zuberi, viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa wakiongozwa na ugeni maalum kutoka kwa Sheikh Mkuu wa Msikiti wa Makkah na Madina Abdul Rahman Al Sudas.
No comments:
Post a Comment