Zimepita siku chache baada ya Spika Job Ndugai kuwasimamisha wasihudhurie Bunge hadi mwakani, mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Ester Bulaya wa Bunda Mjini wote wa Chadema wamefunguka ya moyoni na kumtolea uvivu spika huyo kwamba asidhani yupo juu ya sheria huku wakiahidi kutinga mahakamani kuidai haki yao.
Halima Mdee, amesema Ndugai na wabunge wa CCM lazima waelewe kwamba bunge linaongozwa kwa sheria na kwa sababu hii si mara ya kwanza wao kusimamishwa, watakwenda mahakamani kuhakikisha haki inapatikana.
Aidha Mdee amesisitiza kuwa licha ya kwamba Spika Ndugai alionya kwamba wasiende mahakamani, wao hawaogopi na kwamba wakishinda watashinda pakubwa.
No comments:
Post a Comment