Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema atatuma mkaguzi kuchunguza hali ya upatikanaji na usambazaji wa dawa kwenye zahanati na kituo cha afya cha mjini Gairo, Mkoani Morogoro.
Waziri Majaliwa ametoa Ahadi hiyo alipokuwa akihutubia wakazi wa mji wa Gairo na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Gairo A.
Waziri Mkuu alifikia uamuzi huo baada ya kupata malamiko kutoka kwa wananchi, kuhusiana na uhaba mkubwa wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya.
No comments:
Post a Comment