Msanii wa Bongo Fleva kutoka Label ya WCB, Lava Lava amekanusha uvumi ulioenea kuwa aliwahi kutimuliwa THT na kusema uongozi wake huo wa zamani ulitoa fursa kwa kila msanii kutafuta meneja.
Mwimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Tuachane’ amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds Fm kuwa baada ya kutolewa fursa hiyo ndipo alipotimukia WCB.
“THT sijafukuzwa, kuna muda ulifika tulipewa option ya kumtafuta meneja wa kukusimamia, kwa hiyo mimi kama kijana ambaye ninaendelea kutafuta maisha ilinibidi nitafute mahali ambapo muziki unaweza kusimamiwa,” amesema Lava Lava.
Jumatano hii katika kipindi cha Papaso cha TBC FM, Lava Lava alibainisha kuwa alikaa THT ndani ya miaka mitano kabla ya kutimukia WCB.

No comments:
Post a Comment