Latest News

Thursday, June 8, 2017

Starz Na Lesotho Ni Chamazi Usiku!


Habari kubwa ya michezo baada ya Yanga kushindwa michuano ya Sports Pesa, ni ya mchezo wa kwanza wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya wenyeji, Tanzania ‘Taifa Stars’ na Lesotho ‘Mamba’ ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Jumamosi kuanzia Saa 2:00 usiku.


Hayo yamesemwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi jana usiku katika mahojiano maalum na Bin Zubeiry Sports – Online.
Na Malinzi amesema sababu za mchezo huo kufanyika Uwanja wa klabu ya Azam ni kutokana na Uwanja wa Taifa kuwa katika matengenezo madogo.

Rais Malinzi amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Jumamosi Azam Complex, kuisapoti timu yao ili iweze kufanya vizuri, ambapo Taifa Stars itaingiaa kwenye mchezo huo ikitoka kwenye kambi ya wiki moja mjini Alexandria, Misri.


Nahodha Mbwana Ally Samatta hakuwepo Misri na anatarajiwa kuungana na wenzake hapa Dar es Salaam akitokea Ubelgiji ambako anachezea klabu ya KRC Genk, huku Kiungo wa DC Tenerife ya Hispania, Farid Mussa na mshambuliaji wa AFC Eskilstuna ya Denmark, Thomas Ulimwengu wao walikuwepo Misri na wako tayari kwa mchezo wa keshokutwa.

No comments:

Post a Comment