Watu wengi wamekuwa wakizungumza ya kwao kuhusiana na Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kumteua Mama Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Uteuzi wa Rais Magufuli umewashitua wengi kutokana na Mama Anna Elisha Mghwira kuwa ni mwenyekiti wa chama cha ACT
Wazalendo na aligombea Urais wa Tanzania katika
uchaguzi Mkuu 2015, hivyo wengi wanajiuliza atakubali nafasi hiyo na kama
atakubali atatekeleza ilani ya chama gani CCM au ACT. Baada ya maswali kuwa mengi kwa mmoja kati ya viongozi wa chama
cha ACT Wazalendo na Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameamua kutumia
ukurasa wake wa facebook kuwataka watu kuwa na subira watatoa majibu.
“Nimekuwa naulizwa Sana
kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti wa Chama chetu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Nimekuwa kimya Kwa sababu tumepokea Taarifa za uteuzi kutoka katika vyombo vya
Habari. Mwenyekiti yuko nje ya nchi na kutokana na tofauti za masaa bado
hatujawasiliana nae”
“Tutatoa tamko kamili atakapokuwa amerejea
nchini. Ninawataka wanachama wote wa Act Wazalendo wawe
watulivu na Kama kuna masuala yanayohusu maamuzi ya vikao vya Chama
tutawajulisha. Aliyeteuliwa
ni Mwenyekiti wa Chama Taifa, sio mshauri au mwanachama tu”
“Ni mmoja wa viongozi wa juu wa Chama chetu. Uteuzi wake unahitaji
kikao cha Kamati Kuu ya Chama kukaa na kujadili. Nitaweza kutoa Taarifa baada
ya vikao vya Kamati Kuu ya Chama. Kwa sasa umma usubiri vikao Kwa mujibu wa
Katiba ya Chama chetu”
Mwenyekiti wa ACT
Wazalendo anakuwa mtu wa tatu kutoka cha cha upinzani kuteuliwa na
Rais Magufuli baada ya Augustino Mrema wa TLP kuteuliwa
kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole na Prof Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji.
No comments:
Post a Comment