Latest News

Showing posts with label Habari za Njombe. Show all posts
Showing posts with label Habari za Njombe. Show all posts

Tuesday, May 31, 2016

Wananchi mkoani Njombe wameombwa kutoa hofu kuhusu kuwepo kwa vitendo vya kutowesha amani vikiambatana na mauaji...Nina habari yote!


Jeshi la polisi mkoani Njombe limewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kwa kutoa taarifa mara wanapobaini viashiria vya uwepo wa uhalifu katika maeneo yao ili kuendelea kulinda afya za raia na mali zao.

Picha juu haihusiani na habari...

Rai hiyo imetolewa na kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Njombe John Charles Temu wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kueleza kuwa wananchi wanajukumu la kuripoti taarifa mapema ili kuliwezesha jeshi hilo kukabiliana na vitendo vya kiuhalifu vinavyofanywa na baadhi ya watu wasio waadilifu.
Kauli ya kaimu kamanda huyo imekuja kufuatia tukio la kuuawa kwa jambazi mmoja katika tarafa ya Makambako wilaya ya Njombe mkoani hapa wakati wakikabiliana na askari waliokuwa kwenye doria ambaye mpaka sasa hajafahamika jina lake huku ikielezwa kuwa taarifa za kuwepo kwa uhalifu huo zilitolewa na raia wema.
Kwa mujibu wa kaimu kamanda askari waliokuwa kwenye doria walipambana na majambazi watatu na kufanikiwa kumjeruhi mmoja ambaye mpaka sasa amepoteza maisha na wengine kukimbia huku wakifanikiwa silaha aina ya Long Rifle carber 22mm yenye namba za usajili A 194300 ikiwa na risasi tano ndani ya magazine hiyo.

Temu amesema kuwa kwa sasa hali ya mkoa iko salama na kwamba jeshi la polisi bado linaendelea na msako wa kuwabaini majambazi wawili waliokimbia.

Wananchi Njombe watuhumu taasisi mbali mbali kujihusisha na rushwa.....!


Baadhi ya wananchi Mkoani Njombe wamezituhumu taasisi za umma kujihusisha na masuala ya rushwa jambo ambalo wamedai kuwa linapeleka kuzorota kwa utaoji wa huduma bora kwa wananchi wanapohitaji kupata huduma mbalimbalimbali katika ofisi hizo.

Wametoa malalamiko wakati wakizungumza na waandishi wa habari ambapo wameeleza kuwa baadhi ya maofisa wa taasisi hizo wamekuwa wakiwataka kutoa fedha ili kutimiziwa huduma wanazozihitaji ikiwa ni pamoja na kusainiwa mikataba kwenye taasisi za kifedha huku wakiiomba serikali kuangalia kwa upande wa pili suala hilo kwani linasababisha watu wengi kukosa haki zao za msingi.

Akijibia lawama hizo Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Njombe mhe. John Kapokolo ameeleza kuwa vitendo vya Rushwa ni kosa la jinai ambavyo hutendeka baina ya mtoa rushwa na mpokea rushwa na kuwahimiza wananchi wanaokutana na tatizo kama hilo kutoa taarifa mapema ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.


Miongoni mwa mambo yanayopingwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ni pamoja na rushwa, ubadhilifu, urasimu na upotevu wa mapato ya serikali huku akionesha kutokubaliana na vitu vinavyorudisha nyuma uchumi wa taifa.