Latest News

Friday, April 22, 2016

Ile kesi ya bomoa bomoa Dar es salaam leo majibu yake yamepatikana

Bomoabomoa iliyoanza  mwishoni mwa mwaka 2015 kwenye baadhi ya maeneo jijini Dar es salaam hasa ya mabondeni ikiwemo maeneo yaliyo kando na mto msimbazi ambapo zoezi hilo lilisitishwa baada ya kesi inayopinga
ubomoaji wa nyumba takribani 2619 za wakazi wa Tabata Segerea kufunguliwa.
April 22 2016 yametolewa maamuzi ya kesi hiyo ambapo Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi imesema kwamba kesi hiyo imekosa vigezo vya kisheria kutokana na kutokuwa na kibali cha wananchi wote kwa pamoja kinachoruhusu watu nane kufungua kesi badala ya wananchi wote.
Diwani kata ya Tabata, Patrick Assenga na wakili upande wa utetezi Abubakar Salim wamesema haya …..
>>>mahakama ya juu itafsiri nini maana ya kifungu kile wanaposema ridhaa ya watu, maombi haya yameondolewa sio kwamba yamefutwa sasa maombi yakiondolewa tunaweza tukayaleta tena, kwahiyo tunaweza tukaenda tukaongeza hayo maneno wanayosema hayapo tukarudisha tena au tunaweza watu wote hawa 2619 wafungue kesi moja ambayo itakuwa ni ngumu, tutajipanga tujue nini tufanye kati ya hayo matatu:-Abubakar Salim
>>>’wamesema kuna kasoro za kisheria zimejitokeza ambazo zimesababisha tukakosa uhalali huo, sisi tunaenda kujipanga tutarudisha hii kesi kwa sababu nyumba 2619 ni watu wengi sana ambapo kuna takribani ya watu elfu arobaini na kitu hao watakosa makazi, Rais lazima aingilie kati ni suala kubwa na limebeba maslahi ya watu wengi’:-Patrick Assenga.
Chanzo: Millardayo.

No comments:

Post a Comment