Latest News

Friday, April 22, 2016

Waziri Majaliwa ametoa maagizo kuhusu kero ya elimu nchini.....


Bunge la 11 limeendelea tena leo April 22 2016, Waziri mkuu Kassim Majaliwa amehutubia bunge kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu
kwa mwaka 2016/2017.
Katika kitengo cha huduma ya Jamii Elimu, Waziri Majaliwa amesema ‘Kwa kutambua umuhimu wa Elimu kama nyenzo imara ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, Serikali imeanza kuboresha na kuimarisha elimu ya awali, msingi, sekondari, ufundi na elimu ya juu.’
Baada ya kuanza utekelezaji wa mpango wa elimu bila malipo, kumejitokeza changamoto kadhaa, ikiwemo miundombinu kama madarasa, mabweni, maabara, nyumba za walimu na vyoo‘ ;-Waziri Mkuu Majaliwa
Napenda kuwahakikishia wananchi kwamba Serikali inaendelea kuzifanyia kazi changamoto hizo na jitihada kubwa zimewekwa‘ ;-Waziri Mkuu Majaliwa
Nitumie nafasi hii kuwashukuru wadau walioanza kuchangia madawati katika maeneo mbalimbali,na niwasihi wengine waendelee kuunga mkono Serikali yao‘ ;-Waziri Mkuu Majaliwa
Kuanzia leo hii, nawaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote waliokamata mbao ndani ya Halmashauri zao kuzitumia kutengeneza madawati na siyo kuzipiga mnada‘ ;-Waziri Mkuu Majaliwa
Hali ya urejeshaji wa mikopo iliyotolewa hairidhishi, Hivyo naagiza Bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu kufuatilia urejeshaji wa mikopo hiyo ili fedha hizo zitumike kuwakopesha wanafunzi wengine‘ ;-Waziri Mkuu Majaliwa

No comments:

Post a Comment