Aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam ambaye jana
alisimamishwa kazi na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa
Tanzania, Wilson Kabwe ametaka uchunguzi ufanyike
ili kubaini ukweli kwamba amehusika na ubadhirifu uliotajwa jana na mkuu
wa Mkoa Paul Makonda ama la.
Bwana Kabwe ameliambia gazeti la Mwananchi kuwa,
amekubaliana kusimamishwa kazi kwa kuwa Rais ni bosi wake na
yupo tayari kwa uchunguzi dhidi yake.
“Nimekwambia sina la kukwambia ila niseme tu sina shida na hilo,
uchunguzi ufanyike nina uhakika ukweli utajulikana tu lakini kama
ukijulikana ikibainika nimeonewa kuna fidia yoyote nitalipwa?”
aliuliza.
No comments:
Post a Comment