Latest News

Wednesday, April 20, 2016

Chris brown amefunguka kuwa alitaka kujiua kwa sababu ya Rihanna!


Msanii wa RNB duniani Chris Brown, anatarajia kuachia Documentary itakayohusu maisha yake hivi karibuni ambayo atazungumza kwa uwazi zaidi kuhusu safari yake ya kimuziki na maisha kwa ujumla.
Katika kipande kifupi cha makala yake ya
‘Karibu katika maisha yangu’,mwanamuziki huyo amesema kuwa uhusiano wao ulikuwa kama ndoto lakini akajihisi kama hayawani.
”Nilikuwa katika kilele cha dunia,nyimbo zangu zikiongoza,nikapendwa na wengi nchini Marekani kabla ya kuanguka hadi kuwa adui wa uma”,alisema.
Brown alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kufuata shambulio hilo.
Kifungo hicho kilisitishwa mwaka jana baada ya jaji moja kusema kuwa nyota huyo amekamilisha mahitaji yake yote na kufunga kesi hiyo rasmi.
Makala hiyo inayowaonyesha Jennifer Lopez,Usher,Mike Tyson,Jamie Fox na Rita Ora,Chris Brown anasema kuwa ”Nilihisi kama nyota ,lakini nilijiharibia”.
”Nilikuwa nikilala.Sikuweza kula,nilijihisi maarufu”,alikiri.

No comments:

Post a Comment