Latest News

Wednesday, April 20, 2016

Ulikua unajua kua Dogo janja amokopi biti ya wimbo wa My life?, Mwenyewe kafunguka na wimbo alioukopi ninao hapa tayari


Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ni mdogo bado kiumri Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ anadaiwa kuiba mdundo biti ya mwanamuziki maarufu wa Reggae
kutoka Norway, Philip Boardman ‘Admiral P’ na kuitumia katika wimbo wake mpya wa My Life.

Kwa mujibu wa chanzo, biti hiyo imeibiwa katika Ngoma ya Hatere ya Admiral akimshirikisha Onkl P.

Wimbo huu unapatikana katika albamu ya Admiral ya Selvtillit & Tro.
Dogo janja alipiga stori na Risasi Vibes akafunguka;“Ninachojua mmiliki wa hiyo biti ni Carl Hovind ambaye ni raia wa Norway na amenithibitishia ndiye mmiliki halali wa hiyo biti na kule kwao mmiliki ni prodyuza,” alisema Dogo Janja.

Wimbo wenye hiyo biti ni huu apa...

No comments:

Post a Comment