Latest News

Wednesday, April 20, 2016

Bifu ya Wizkid na Linda Ikeji limeisha!!!


Nikukumbushe kidogo kuhusu bifu ya mastaa Linda pamoja na Wizkid, ishu ilianzia kwenye blog ya Linda baada ya kuandika kuwa msanii huyo amepewa notice na mmiliki wa nyumba aliyokuwa amepanga kuhama kwasababu ameshindwa kulipia kodi ya pango. Hatua hiyo
ilimfanya Wizkid amshambulie blogger huyo kwa lundo la matusi kwenye Instagram ikiwemo kumtisha kumpiga.
Linda alikuwa amepanga kufungua kesi polisi kwa kudai maisha yake yapo hatarini. Hata hivyo wawili hao walikutana polisi wikiendi iliyopita jijini Lagos na kumaliza kesi yao bila kushtakiana.
“I spoke with Wizkid through his lawyer on Friday April 15, 2016 where he tendered an apology to me and said he wasn’t a violent person, that he didn’t mean what he said, that it was just an emotional outburst. And then he asked for forgiveness,” alisema Linda.
Wizkid alienda kwenye kituoni akiwa na wanasheria watatu na meneja wake, Sunday Are. Alishare picha Instagram akiwa polisi na kuandika: With the Hon Commissioner of Lagos Police!!! Police is ur friend #youngPablo!!”
Akiongea kwanini hakupiga picha na Wizkid kituoni hapo, Linda alisema: I turned down taking a photo with him and the police commissioner this afternoon. One of his people took a pic of him and the commissioner with me in it and my people insisted they delete it. Not because I haven’t forgiven him, I just don’t need the extra drama.”

No comments:

Post a Comment