Kuna taarifa za staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo kuhusishwa kutaka kuhama Real Madrid na kutaka kujiunga na klabu ya Paris Saint Germain
ya Ufaransa zimerudi tena katika mitandao.Awali Ronaldo aliwahi kuhusishwa kutaka kujiunga na PSG ila leo April 19 2016 stori kutoka 101greatgoals.com wameripoti kuwa Cristiano Ronaldo amewahi kukutana na Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi mara tano, stori zinaeleza kuwa Jose Mourinhohuenda akajiunga na PSG pamoja na Ronaldo msimu ujao.
Taarifa za Ronaldo kukutana na Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi zimevuja baada yaRonaldo kudaiwa kuonekana akiwa Paris Ufaransa kwa ndege ya kukodi na kupelekwa katika hoteli aliyopo Nasser Al-Khelaifi na siku inayofuatia Ronaldo anadaiwa kuondoka na ndege binafsi tena kuwahi mazoezi ya Real Madrid. Huenda kukawa kuna kitu kinaendelea kwani Ronaldo amekuwa akionekana Paris mara kadhaa sasa.
No comments:
Post a Comment