Kuna taarifa zimenifikia hapa kuhusu watu wawili kufariki dunia alfajiri ya leo baada ya gari aina ya Toyota Hiace namba T271 CRG kuserereka wakati likiingia katika kivuko cha feri (ambacho kimekuwa kikitumika miaka yote) na kutumbukia
baharini leo eneo la Kivukoni jijini Dar es Salaam.
baharini leo eneo la Kivukoni jijini Dar es Salaam.
Waliofariki kutokana na ajali hiyo ni; Dereva la gari hilo mwanaume aliyetambulika kwa jina moja la Daniel (anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30-35) mkazi wa Dar es Salaam ambaye aliokolewa amapema asubuhi ya leo na mwingine ni mwanamke aliyetambulika kwa jina la Nice Mwakalinga mwenye umri wa miaka 52 mkazi wa Tukuyu Masoko mkoani Mbeya.
Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa marehemu hao, marehemu Daniel ameacha mtoto mmoja na marehemu Nice ameacha watoto watano.
Tayari miili ya marehemu wote imepatikana na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ili taratibu zingine za mazishi zifanyike.
Kaka ambaye ni manusura wa ajali hiyo anasema, ndugu hao waliotumbukia kwenye gari akiwemo dada yake Nice kwa pamoja walikuwa wakitokea mkoani Mbeya kwenye msiba.
Tukio hili limetokea ikiwa ni siku moja tu baada ya rais john Pombe Magufuli kuzindua daraja jipya la Kigamboni (Nyerere Bridge) ambalo linatumika kwa ajili ya magari, waenda kwa miguu na baiskeli.
Tizama picha hapa chini:-
No comments:
Post a Comment