Latest News

Wednesday, April 20, 2016

Wasanii wa kike wa Hiphop sio lazima tuishi kigumu, Pink!


Kuna baadhi watoto wa kike wamekuwa na mwonekano wa kigumu, yaani maisha na mwonekano fulani kama wa kiume hususan baadhi ya wasanii wa kike
wanaoimba Hiphop Bongo.

Msanii wa kike wa Hihop kutoka hapa 255, anayekwenda kwa jina la Pink amepiga stori na East Africa Radio na akaelezea hili kwa kusema kuwa sio lazima eti kwakuwa unaimba Hiphop ndio uwe na mwonekano wa kigumu, hususan yeye anaimba Hiphop lakini hana mwonekano wa kigumu kama baadhi ya wanamuziki kama Chemical na wale wakongwe kina Ssiter p, Zay b n.k

'Msije mkashangaa siku nimepanda stejini naperfom nimevaa skuna au skirt hivyo ndivyo nilivyoamua mimi kama mimi kwa hiyo sio lazima uishi kigumu kwakuwa unaimba Hiphop'. Alisema Pink.

No comments:

Post a Comment