Latest News

Wednesday, April 20, 2016

Hapa ni kuhusu ishu ya mtoto wa shule ya msingi kulawitiwa mkoani Iringa


Wakazi mkoani Iringa wamelaani vikali kitendo kilichofanywa na jamaa mmoja anayeishi eneo la Tandamti kata ya Makorongoni mkoani Iringa cha kumlawiti mtoto wa kiume
aliyehifadhiwa jina anayesoma shule ya msingi mkoani hapa.


Wakizungumza na kituo cha redio cha Ebon Fm Iringa wakazi waliokuwepo eneo hilo wamesema walimwona kijana mtuhumiwa akiingia na mtoto huyo kwenye nyumba ambayo ilikua haikaliwi na watu na hatimaye ikagundulika jamaa huyo alikua ameandaa sehemu maalum kwenye nyumba hiyo kwaajili ya kitendo hicho cha kinyama na pia alikua na mafuta ambayo aliyatumia kwenye dhambi hiyo.

Inasemekana mtoto huyo ana umri wa miaka kama sita hivi na ndio mara yake ya kwanza kufanyiwa hivyo, mtoto huyo alidanganywa kuwa anombwa akasaidiwe kubeba ngazi kabla ya tukio kufanyika.

Hata hivyo mwenye nyumba hiyo ndiye aliyegundua tukio mara baada ya kuja na kukuta mlango umefungwa kwa ndani na alipogonga kwa nguvu ndipo alipojitokeza huyo kijana akiwa na wasi wasi mwingi hatimaye mwenye nyumba huyo akamfungia kwa nje na kwenda kuripoti kwenye uongozi wa mtaa na hatimaye waliwasiri na kumhoji kijana kuhusu nia ya kufunga mlango.

Mzazi wa mtoto huyo alikuwa na jazba sana baada ya kupata taarifa hizo ingawa kilichofanyika ni kumfikisha kwenye kituo cha polisi.

Wananchi wa eneo hilo wanasema hilo tukio sio la kwanza kwahiyo haliwashangazi sana.

No comments:

Post a Comment