Mchezaji maarufu duniani Lionel Messi amesema hafahamu jambo lolote kwejye mikataba anayosaibi kwa sababu huwa hana utaratibu wa kusoma.
Kauli hii ya Lionel Messi inakuja wakati kesi yake ya ukwepaji kofi inatarajiwa kuendelea Jumanne ya leo, Katika kesi hiyo Messi na Baba yake Jorge Horacio wanatuhumiwa kukwepa kodi ya kiasi cha 4.1 million euros katika kipindi cha baina ya 2007 na 2009.
Kwa mujibu wa gazeti la Catalan la El Periodico, Messi alimwambia jaji mwaka 2013: “Namuamini baba yangu, ambaye anashughulikia biashara zangu zote. “Chochote anachoniambia nifanye, nafanya.”
Alipoulizwa kama huwa anasomaga mikataba yake kabla ya kusaini, nahodha huyo wa Argentina.
“Nasaini kila kitu lakini sijawahi kusoma mikataba.
“Sijui nini nasaini.”
Baada ya ratiba ya leo ya kesi Messi anatarajiwa kurudi kujiunga na timu yake ya taifa ya Argentina kwa ajili ya michuano ya Copa America inayotarajiwa kuanza tarehe 4, June.
No comments:
Post a Comment