Latest News

Saturday, June 25, 2016

"Suala la usalama halina vyama", Rais Magufuli


Rais John Magufuli amezindua Mpango wa Usalama wa Jamii akisema Watanzania wana imani na Jeshi la Polisi na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.
Rais Magufuli pia amesema kwamba suala ujambazi, halina vyama vya siasa na kushangaa kutomwona Meya wa Kinondoni (Chadema), Boniface Jacob.
Vilevile  Rais Magufuli amesema yeye  hatumbui watu, bali watu hao wanajitumbua wenyewe kutokana na makosa na dhambi zao wanazozitenda.
Ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kushirikiana kikamilifu na Jeshi la Polisi ili kurahisisha mawasiliano ya simu zitakazokuwa zikipigwa na wananchi.
Vilevile alimuagiza Katibu Mkuu Kiongozi, BaloziJohn Kijazi kuwaambia TCRA kutelekeza agizo hilo na asiyetaka kufanya aondoke kwa sababu mamlaka hiyo ni sehemu ya Serikali.
Pia aliahidi kulitafutia helkopta mpya jeshi hilo itakayowasaidia katika shughuli zao za kila siku.

No comments:

Post a Comment