Luteni Mstafu Chifu Ghalawa amesema serikali ipo tayari kuendelea kuimarisha mipaka ya Tunduma na Ileje kwa lengo la kuimarisha mipaka ya nchi.
Ghalawa ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini songwe ambapo amesema hatua hiyo itasaidia kukomesha biashara za magendo.
Mipaka ya Tunduma na ileje ni miongoni mwa mipaka iliyo na mchango mkubwa wa mapato ya taifa, serikali ya mkoa mpya wa songwe imejizatiti kuboresha mazingira ya mipaka hiyo ili iwe rafiki kwa watumiaji wa ndani ya nchi na nje.
Mkoa wa Songwe ndio umekwisha anzishwa tayari na umekuwa na fursa kwa ajili ya kuongeza mapato kwa kukuza uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja wa maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment